Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • ‘Kwani Nina Shida Gani?’
    Amkeni!—2004 | Julai 8
    • Wakati wa kubalehe wasichana huanza kupata kipindi cha hedhi, ambacho hutukia kila mwezi na kinahusisha kutokwa damu, umajimaji, na mabaki ya chembe kutoka kwenye tumbo la uzazi.a Kwa kawaida katika kipindi cha hedhi mtu huwa na mkakamao na viwango vyake vya homoni hupungua. Kwa kuwa hilo huathiri mwili na hisia, mwanzo wa kipindi cha hedhi unaweza kusababisha wasiwasi mwingi. Teresa, ambaye sasa ana umri wa miaka 17, anakumbuka hivi: “Ghafula, nililazimika kukabiliana na hali mpya. Ilivuruga hisia zangu na kuniumiza. Na ilitukia kila mwezi!”

      Hakuna haja ya kuogopa unapoanza kupata vipindi vya hedhi. Vipindi hivyo vinaonyesha kwamba mwili wako unafanya kazi vizuri. Muda si muda, utajua jinsi ya kukabiliana na magumu ya vipindi hivyo. Kwa mfano, wengine wameona kwamba kufanya mazoezi kwa ukawaida hupunguza hali ya kukakamaa. Lakini kila mtu ni tofauti. Huenda ukagundua kwamba unahitaji kupunguza sana utendaji wako wa kimwili wakati wa vipindi hivyo. Jifunze kutambua mahitaji ya mwili wako na kuyatosheleza.

  • ‘Kwani Nina Shida Gani?’
    Amkeni!—2004 | Julai 8
    • a Mwanzoni, vipindi vya hedhi vinaweza kutukia zaidi ya mara moja au chini ya mara moja kwa mwezi. Kiasi cha mtiririko kinaweza kutofautiana sana pia. Hali hizo hazipaswi kukushtua. Hata hivyo, vipindi vya hedhi visivyo vya kawaida vikiendelea kwa mwaka mmoja au miwili, huenda ikafaa kumwona daktari.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki