Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Réunion
    2007 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
    • MAHALI PA KUFANYIA MAKUSANYIKO YA MZUNGUKO

      Kazi ya kuhubiri kisiwani Réunion ilifanikiwa sana hivi kwamba ilikuwa vigumu kupata mahali pakubwa vya kutosha kufanyia makusanyiko. Katika 1964, ndugu walipanga kusanyiko lao la kwanza la mzunguko. Walitafuta kwa miezi kadhaa mahali pa kufanyia kusanyiko nao wakapata mkahawa mmoja uliokuwa ghorofani huko Saint-Denis. Jengo hilo la zamani lilikuwa limejengwa kwa mbao na lilikodishwa pesa nyingi. Wenye jengo hilo walisema lingeweza kustahimili uzito wa watu 200 ambao tulitarajia wahudhurie.

      Ndugu hawakuwa na lingine ila kukodi mkahawa huo. Mtu fulani mwenye mwelekeo mzuri alitupa mfumo wa vipaza-sauti. Siku ilipofika ndugu walijaa katika jengo hilo, na ingawa sakafu yake ilitoa sauti kubwa ya mkwaruzo, haikuporomoka. Watu 230 walihudhuria siku ya Jumapili, na 21 wakabatizwa.

      Punde baadaye, kwa fadhili Louis Nelaupe, yule ndugu aliyekulia Cirque de Mafate, alitoa sehemu ya kiwanja chake huko Saint-Denis kwa ajili ya ujenzi wa Jumba la Kusanyiko la muda. Jumba hilo lililojengwa kwa nguzo za mbao na kuezekwa kwa mabati lilikuwa na kuta za makuti yaliyosokotwa.

      Kusanyiko la kwanza kufanyiwa huko lilikuwa la siku tatu. Myriam Andrien aliyehudhuria kusanyiko hilo anasema: “Asubuhi siku ya kwanza, tulienda kuhubiri na kurudi kula chakula moto cha mchana cha Krioli, ambacho ni wali, maharagwe, na nyama ya kuku iliyotiwa pilipili kali. Wale ambao hawajazoea pilipili kali walipikiwa mchuzi unaoitwa rougail marmaille, usio na pilipili nyingi.”

      Wahudhuriaji walipoongezeka, Jumba la Kusanyiko lilipanuliwa, nalo lilitumiwa pia kama Jumba la Ufalme. Baadaye, familia zilizokodi nyumba ambazo zilikuwa kwenye kile kiwanja zilihama, na Louis akalikabidhi kutaniko kiwanja chote. Sasa eneo hilo lina Jumba la Ufalme zuri la matofali linalotumiwa na makutaniko mawili ya Saint-Denis.

  • Réunion
    2007 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
    • Jengo la muda la kufanyia mikutano huko Saint-Denis mnamo 1965

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki