-
Réunion2007 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
-
-
Mwaka mmoja hivi baadaye, ndugu katika kikundi hicho kipya jijini Saint-Denis walikodi ukumbi mdogo uliotoshea watu 30 hivi. Ukumbi huo uliojengwa kwa mbao na kuezekwa kwa mabati, ulikuwa na madirisha mawili na mlango mmoja. Baada ya kupata kibali, ndugu walibomoa kuta za ndani, wakajenga jukwaa dogo, na kuweka viti visivyo na sehemu ya kuegemea.
Siku za Jumapili wakati jua lilipowaka asubuhi, paa hilo la mabati lilifanya ukumbi huo uwe na joto jingi. Baada ya muda, wote waliokuwa ndani walitokwa na jasho, hasa wale waliosimama jukwaani, vichwa vyao vikiwa karibu na paa. Isitoshe, kwa kuwa mara nyingi ukumbi huo ulijaa kabisa, watu wengi walisikiliza wakiwa kwenye madirisha na mlango, na kufanya waliokuwa ukumbini wakose hewa safi.
-
-
Réunion2007 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
-
-
Myriam Andrien alikuwa mmoja wa wanafunzi hao wapya, naye alianza kujifunza alipokuwa Madagaska mwaka wa 1961. Anakumbuka ukumbi huo ulitumiwa pia kama Jumba la Kusanyiko. Ndugu walipanua sehemu ya kuketi kwa kujenga kibanda cha makuti.
-