-
Réunion2007 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
-
-
MAHALI PA KUFANYIA MAKUSANYIKO YA MZUNGUKO
Kazi ya kuhubiri kisiwani Réunion ilifanikiwa sana hivi kwamba ilikuwa vigumu kupata mahali pakubwa vya kutosha kufanyia makusanyiko. Katika 1964, ndugu walipanga kusanyiko lao la kwanza la mzunguko. Walitafuta kwa miezi kadhaa mahali pa kufanyia kusanyiko nao wakapata mkahawa mmoja uliokuwa ghorofani huko Saint-Denis. Jengo hilo la zamani lilikuwa limejengwa kwa mbao na lilikodishwa pesa nyingi. Wenye jengo hilo walisema lingeweza kustahimili uzito wa watu 200 ambao tulitarajia wahudhurie.
Ndugu hawakuwa na lingine ila kukodi mkahawa huo. Mtu fulani mwenye mwelekeo mzuri alitupa mfumo wa vipaza-sauti. Siku ilipofika ndugu walijaa katika jengo hilo, na ingawa sakafu yake ilitoa sauti kubwa ya mkwaruzo, haikuporomoka. Watu 230 walihudhuria siku ya Jumapili, na 21 wakabatizwa.
-
-
Réunion2007 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
-
-
watu 230 wahudhuria kusanyiko la kwanza la mzunguko kisiwani Réunion.
-
-
Réunion2007 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
-
-
1998 Kusanyiko la kwanza lafanywa katika Jumba jipya la Kusanyiko huko La Possession.
-
-
Réunion2007 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
-
-
[Picha katika ukurasa wa 251]
Makusanyiko
Kusanyiko la kwanza la mzunguko kisiwani Réunion lilifanywa katika mkahawa uliokuwa ghorofani mnamo 1964
Mahali panapoitwa “Pango la Wafaransa wa Kwanza” ambapo kusanyiko la wilaya lilifanyiwa
Jengo la muda la kufanyia mikutano huko Saint-Denis mnamo 1965
-