Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Kazi za Yehova—Kubwa na za Ajabu
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • “Na baada ya vitu hivi mimi nikaona, na patakatifu pa hema ya ushahidi palifunguliwa katika mbingu, na malaika saba wakiwa na tauni saba waliibuka kutoka patakatifu, wakiwa wamevaa kitani safi, nyangavu na wamefunga kifuani mishipi ya dhahabu. Na mmoja wa viumbe hai wanne akawapa malaika saba mabakuli saba ya dhahabu yaliyokuwa yamejaa kasirani ya Mungu, ambaye huishi milele na milele.”—Ufunuo 15:5-7, NW.

      15. Kwa nini haishangazi kwamba malaika saba huibuka kutoka patakatifu?

      15 Kwa habari ya hekalu la Israeli, ambalo lilikuwa na viwakilishi vya vitu vya kimbingu, ni kuhani mkuu pekee angeweza kuingia Patakatifu Zaidi Sana, panapoitwa hapa “patakatifu.” (Waebrania 9:3, 7, NW) Panawakilisha kuwapo kwa Yehova katika mbingu. Hata hivyo, katika mbingu yenyewe, si Kuhani Mkuu Yesu Kristo tu aliye na pendeleo la kuingia mbele za Yehova bali pia malaika hufanya hivyo. (Mathayo 18:10; Waebrania 9:24-26) Basi, haishangazi kwamba malaika saba wamepaswa kuonekana wakitoka katika patakatifu katika mbingu. Wao wana utume kutoka kwa Yehova Mungu mwenyewe: Mimineni mabakuli yanayojaa kasirani ya Mungu.—Ufunuo 16:1, NW.

  • Kazi za Yehova—Kubwa na za Ajabu
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • Yehova Katika Patakatifu Pake

      17. Yohana hutuambia nini sasa juu ya patakatifu, na hilo hutukumbushaje sisi juu ya patakatifu katika Israeli wa kale?

      17 Mwishowe, akimaliza sehemu hii ya njozi, Yohana anatuambia: “Na patakatifu pakajawa na moshi kwa sababu ya utukufu wa Mungu na kwa sababu ya nguvu zake, na hakuna mmoja ambaye aliweza kuingia ndani ya patakatifu mpaka tauni saba za malaika saba zilipokuwa zimekwisha.” (Ufunuo 15:8, NW) Kulikuwako vipindi katika historia ya Israeli wakati wingu lilifunika patakatifu halisi, na udhihirisho huu wa utukufu wa Yehova ulizuia makuhani kuingia humo. (1 Wafalme 8:10, 11; 2 Nyakati 5:13, 14; linga Isaya 6:4, 5.) Hizi zilikuwa nyakati Yehova alipokuwa anahangaikia sana matukio duniani.

      18. Hao malaika saba watarudi lini kutoa ripoti kwa Yehova?

      18 Vilevile, sasa Yehova anapendezwa sana na vitu vinavyotukia duniani pia. Yeye anataka malaika saba watimize mgawo wao. Ni wakati wa upeo wa hukumu, kama inavyoelezwa kwenye Zaburi 11:4-6, NW: “Yehova yumo katika hekalu takatifu lake. Yehova—kiti cha ufalme chake kimo katika mbingu. Macho yake mwenyewe huona, macho yake mwenyewe yenye kung’aa huchunguza wana wa binadamu. Yehova mwenyewe huchunguza mwadilifu na pia mwovu na yeyote mwenye kupenda jeuri nafsi Yake hakika huchukia. Yeye atanyesha chini juu ya waovu mitego, moto na salfa na upepo wenye kuunguza, kuwa aria ya kikombe chao.” Mpaka tauni saba hizi ziwe zimemiminwa juu ya waovu, malaika saba hawatarudi kwenye kuwapo kulikotukuka kwa Yehova.

      19. (a) Ni amri gani inayotolewa sasa, na inatolewa na nani? (b) Ni lazima kumiminwa kwa mabakuli ya ufananisho kuwe kulianza lini?

      19 Amri yenye kutia hofu yatokeza mngurumo: “Na mimi nikasikia sauti kubwa kutoka patakatifu ikisema kwa malaika saba: ‘Endeni na kumimina mabakuli saba ya kasirani ya Mungu ndani ya dunia.’” (Ufunuo 16:1, NW) Ni nani anayetoa amri hii? Ni lazima awe Yehova mwenyewe, kwa kuwa mng’aro wa utukufu na nguvu zake ulizuia mwingine yeyote kuingia patakatifu. Yehova alikuja kwenye hekalu lake la kiroho kwa ajili ya hukumu katika 1918. (Malaki 3:1-5) Basi, lazima iwe ilikuwa muda mfupi baada ya tarehe hiyo kwamba yeye akatoa hiyo amri ya kumimina “mabakuli ya kasirani ya Mungu.” Kwa kweli, hukumu zilizo katika mabakuli ya ufananisho zilianza kupigiwa mbiu kwa mkazo mkubwa katika 1922. Na leo ukubwa wa sauti za mbiu yao unazidi kuongezeka.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki