-
Unapima Mafanikio Jinsi Gani?Mnara wa Mlinzi—2007 | Januari 1
-
-
Unapima Mafanikio Jinsi Gani?
JESSE LIVERMORE, alionwa na watu fulani kuwa mfanyabiashara aliyefanikiwa zaidi katika soko la hisa la Wall Street. Alijulikana kuwa mtu aliyefanya maamuzi ya kibiashara yenye hekima. Kwa hiyo, alitajirika sana. Alivalia suti nzuri sana zilizoshonwa kwa mikono. Aliishi katika nyumba kubwa yenye vyumba 29, naye alitumia gari jeusi la kifahari aina ya Rolls-Royce na alikuwa na dereva wake.
-
-
Unapima Mafanikio Jinsi Gani?Mnara wa Mlinzi—2007 | Januari 1
-
-
Watu wengi wanaamini kwamba kufanikiwa ni kupata utajiri, sifa, au umaarufu. Hata hivyo, wale walio matajiri huenda bado wanahisi kwamba maisha yao ni matupu na hayana kusudi. Bwana Livermore alihisi hivyo. Ingawa alikuwa tajiri, maisha yake yalikuwa yenye kuvunja moyo sana, yalijaa misiba na huzuni. Alishuka moyo sana, kila ndoa aliyofunga ilivunjika, naye hakuwa na uhusiano mzuri na watoto wake. Mwishowe, baada ya kupoteza utajiri wake mwingi, siku moja Bwana Livermore aliketi katika baa kwenye hoteli fulani ya kifahari na kujisikitikia kwa sababu ya hasara alizopata. Aliomba kinywaji, akatoa kijitabu chake chenye jalada la ngozi na kumwandikia mke wake barua ya kumuaga. Alipomaliza kinywaji, aliingia katika chumba fulani ambacho hakikuwa na mwangaza wa kutosha, kisha akajiua.
-