Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w07 1/1 kur. 3-4
  • Unapima Mafanikio Jinsi Gani?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Unapima Mafanikio Jinsi Gani?
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2007
  • Habari Zinazolingana
  • Jinsi Unavyoweza Kupata Mafanikio ya Kweli Maishani
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2012
  • Kufanikiwa kwa Gharama Yoyote?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1988
  • Jinsi Unavyoweza Kufanikiwa
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2007
  • Jinsi ya Kupata Mafanikio ya Kweli
    Amkeni!—2014
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2007
w07 1/1 kur. 3-4

Unapima Mafanikio Jinsi Gani?

JESSE LIVERMORE, alionwa na watu fulani kuwa mfanyabiashara aliyefanikiwa zaidi katika soko la hisa la Wall Street. Alijulikana kuwa mtu aliyefanya maamuzi ya kibiashara yenye hekima. Kwa hiyo, alitajirika sana. Alivalia suti nzuri sana zilizoshonwa kwa mikono. Aliishi katika nyumba kubwa yenye vyumba 29, naye alitumia gari jeusi la kifahari aina ya Rolls-Royce na alikuwa na dereva wake.

Davida pia alikuwa ameazimia kufanikiwa. Akiwa msaidizi wa mwenyekiti na meneja mkuu wa kampuni kubwa ya uchoraji, alikuwa akikaribia kuwa msimamizi wa idara fulani ya kampuni hiyo. Alivutiwa sana na utajiri na umaarufu. Hata hivyo, David alifanya uamuzi ambao ulimwongoza ajiuzulu. David alisema hivi: “Ninajua kwamba sitapata tena kazi kubwa kama hiyo.” Je, unafikiri David alikosea?

Watu wengi wanaamini kwamba kufanikiwa ni kupata utajiri, sifa, au umaarufu. Hata hivyo, wale walio matajiri huenda bado wanahisi kwamba maisha yao ni matupu na hayana kusudi. Bwana Livermore alihisi hivyo. Ingawa alikuwa tajiri, maisha yake yalikuwa yenye kuvunja moyo sana, yalijaa misiba na huzuni. Alishuka moyo sana, kila ndoa aliyofunga ilivunjika, naye hakuwa na uhusiano mzuri na watoto wake. Mwishowe, baada ya kupoteza utajiri wake mwingi, siku moja Bwana Livermore aliketi katika baa kwenye hoteli fulani ya kifahari na kujisikitikia kwa sababu ya hasara alizopata. Aliomba kinywaji, akatoa kijitabu chake chenye jalada la ngozi na kumwandikia mke wake barua ya kumuaga. Alipomaliza kinywaji, aliingia katika chumba fulani ambacho hakikuwa na mwangaza wa kutosha, kisha akajiua.

Ijapokuwa watu wanajiua kwa sababu mbalimbali, kisa hiki kinathibitisha kwamba maneno haya ya Biblia ni ya kweli: “Wale ambao wameazimia kuwa matajiri . . . wamejichoma wenyewe kila mahali kwa maumivu mengi.”—1 Timotheo 6:9, 10.

Je, inawezekana kwamba wale wanaofikiri kuwa kufanikiwa ni kupata utajiri, cheo, au umaarufu wanapima mafanikio kwa njia isiyofaa? Je, unajiona kuwa umefanikiwa? Kwa nini unafikiri hivyo? Unapima mafanikio yako jinsi gani? Maoni yako kuhusu mafanikio yanategemea nini? Habari inayofuata itazungumzia mashauri yenye kutegemeka ambayo yamewawezesha mamilioni ya watu kufanikiwa. Acha tuone jinsi wewe pia unavyoweza kufanikiwa.

[Maelezo ya Chini]

a Jina limebadilishwa.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki