Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Rumania
    2006 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
    • Jumba la Kusanyiko Badala ya Jumba la Nyuki

      Hakuna Majumba ya Ufalme yaliyojengwa wakati wa utawala wa Kikomunisti ila tu lile Jumba la Nyuki lililotajwa mapema. Kwa hiyo, marufuku ilipofutwa kulikuwa na uhitaji mkubwa sana wa Majumba ya Ufalme. Katika miaka ya majuzi, mpango wa Hazina ya Majumba ya Ufalme umewawezesha ndugu kujenga kwa wastani Jumba moja la Ufalme kila siku kumi! Majumba hayo yote yasiyo na madoido yanafanana, nayo yamejengwa kwa vifaa vinavyopatikana kwa urahisi. Kama ilivyo katika nchi nyingine, majirani, wafanyabiashara, na wakuu wa miji hutolewa ushahidi kwa mipango mizuri ya ujenzi na roho ya kujitolea ya wajenzi, hasa wakati majumba yanapojengwa kwa muda mfupi.

      Katika Mkoa wa Mureş, ndugu waliwaendea wenye mamlaka ili kupata kibali cha kuweka umeme katika Jumba la Ufalme lililokuwa likijengwa. Ofisa mmoja aliwauliza: “Mna haraka gani? Itachukua angalau mwezi mmoja kushughulikia kibali chenu, na hamtakuwa mmeendelea sana.” Kwa hiyo, ndugu wakamwendea mkurugenzi.

      Yeye pia aliuliza: “Kwani mna haraka gani? Mmetoka tu kuweka msingi, sivyo?”

      Ndugu wakajibu: “Naam, lakini tuliweka msingi juma lililopita, sasa tunaweka paa!” Mkurugenzi alielewa, naye akatoa kibali kesho yake.

  • Rumania
    2006 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
    • [Picha katika ukurasa wa 158]

      (1) Jengo lenye Majumba ya Ufalme matatu, Tirgu-Mures

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki