-
Mungu Yumo Katika Hekalu Lake TakatifuUnabii wa Isaya I—Nuru kwa Wanadamu Wote
-
-
19. Ijapo taifa hilo litakatwa kama mti, Mungu ampa Isaya uhakikisho gani?
19 Hapana shaka kwamba uharibifu utakaoifanya Yuda kuwa “ganjo kabisa” utakuja, lakini hali ni yenye tumaini fulani. (2 Wafalme 25:1-26) Yehova amhakikishia Isaya: “Ijapokuwa imebaki sehemu moja katika sehemu kumi ndani yake, italiwa hii nayo; kama mvinje na kama mwaloni, ambao shina lake limebaki, ingawa imekatwa; kadhalika mbegu takatifu ndiyo shina lake.” (Isaya 6:13) Naam, “sehemu moja katika sehemu kumi . . . mbegu takatifu,” itabaki, kama vile shina la mti mkubwa mno uliokatwa. Yamkini uhakikisho huo wamfariji Isaya—mabaki watakatifu watapatikana kati ya watu wake. Ijapo taifa hilo lachomwa kwa mara nyingine tena, kama mti mkubwa uliokatwa kwa minajili ya kuni, shina muhimu la mti wa ufananisho wa Israeli litabaki. Litakuwa mbegu, au uzao, mtakatifu kwa Yehova. Baadaye, litachipuka tena, na mti huo utakua upya.—Linganisha Ayubu 14:7-9; Danieli 4:26.
20. Sehemu ya mwisho ya unabii wa Isaya ilitimizwaje mwanzoni?
20 Je, maneno ya unabii huo yalitimia? Ndiyo. Miaka 70 baada ya nchi ya Yuda kuharibiwa, mabaki wenye kumhofu Mungu walirudi kutoka uhamishoni huko Babiloni. Walijenga upya hekalu na jiji, nao wakairudisha ibada ya kweli nchini humo. Kurudishwa huko kwa Wayahudi katika nchi yao waliyopewa na Mungu kulifanya utimizo wa pili wa unabii ambao Yehova alimpa Isaya uwezekane. Utimizo huo ulipaswa kuwa nini?—Ezra 1:1-4.
-
-
Mungu Yumo Katika Hekalu Lake TakatifuUnabii wa Isaya I—Nuru kwa Wanadamu Wote
-
-
Ingawa hivyo, baadhi ya watu walikuwa wamemsikiliza Yesu na kuwa wanafunzi wake. Yesu aliwatangaza hao kuwa ‘wenye furaha.’ (Mathayo 13:16-23, 51) Alikuwa amewajulisha kuwa waonapo “Yerusalemu limezingirwa na majeshi yaliyopiga kambi,” yawapasa “[kuanza] kukimbia hadi kwenye milima.” (Luka 21:20-22) Kwa hiyo, “mbegu takatifu” iliyokuwa imedhihirisha imani na iliyokuwa imefanywa kuwa taifa la kiroho, “Israeli wa Mungu,” iliokolewa.a—Wagalatia 6:16.
-