Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Nchi Ambazo Zilikuwa Sehemu ya Yugoslavia
    2009 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
    • Ofisi ya Belgrade ilifungwa, na kazi ya kuwagawia akina ndugu chakula cha kiroho ilipangiwa Zagreb, Kroatia.

  • Nchi Ambazo Zilikuwa Sehemu ya Yugoslavia
    2009 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
    • Huko Serbia, majeshi ya Nazi yalijenga kambi za mateso na kambi za kazi ngumu. Kwa sababu ya msimamo wao wa kutounga mkono upande wowote, ndugu zetu zaidi ya 150 kutoka Hungaria walifungwa katika kambi moja karibu na Bor, Serbia.

  • Nchi Ambazo Zilikuwa Sehemu ya Yugoslavia
    2009 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
    • Stevan Stanković, mfanyakazi wa reli, kutoka Serbia, alikuwa tayari kuwasaidia akina ndugu bila kujali malezi yao. Bila kujali hatari, Stevan alikubali kazi ya kupeleka vitabu kwa siri kutoka Kroatia mpaka nchi ya Serbia iliyokuwa chini ya ulinzi wa wanajeshi. Siku moja polisi waligundua vitabu katika sanduku alilobeba. Walitaka kujua vitabu hivyo vilitoka wapi. Hata hivyo, Stevan alikuwa mshikamanifu kwa ndugu zake, akakataa kuwapa habari hiyo. Polisi walimtia gerezani ili wamhoji halafu wakampeleka kwenye kambi ya mateso ya Jasenovac iliyo karibu. Ndugu yetu mwaminifu aliuawa katika kambi hiyo ambayo ilijulikana sana kwa sababu ya ukatili.

  • Nchi Ambazo Zilikuwa Sehemu ya Yugoslavia
    2009 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
    • MATESO WAKATI WA VITA

      Mnamo Aprili 6, 1941, jeshi la Ujerumani lilishambulia Yugoslavia. Ofisi ya tawi iliharibiwa na ndege za kivita zilizoshambulia sana Belgrade. Wanajeshi wa Ujerumani waliigawanya nchi ya Yugoslavia. Kwa muda fulani, vita vilikatiza mawasiliano kati ya ndugu wa Betheli ya Serbia na ndugu wa Slovenia, Kroatia, na Makedonia.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki