Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Nilijifunza Kumtegemea Mungu
    Amkeni!—2006 | Aprili
    • Kufungwa Kisha Kuhamishwa Hadi Siberia

      Mimi na Alma tulipakia vitu vichache kwa utulivu, kisha tukala. Maofisa hao wa KGB walishangaa na kusema, “Hata hamtoi machozi. Mnaketi tu hapo mkila.” Tuliwajibu, “Tunaenda kwenye mgawo wetu mpya nasi hatujui tutakula lini tena.” Nilibeba blanketi ambayo nilitumia kutengeneza soksi nzito na sweta. Baada ya kufungwa kwa miezi mingi, mnamo Agosti 1951, mimi pamoja na Mashahidi wengine tulihamishwa hadi Estonia.c

      Kutoka Estonia tulihamishwa kwa gari-moshi hadi Leningrad (sasa ni St. Petersburg), Urusi, na kutoka hapo tukapelekwa kwenye kambi zenye sifa mbaya huko Vorkuta, Komi, juu ya Mzingo wa Aktiki. Kulikuwa na Mashahidi watatu katika kikundi chetu. Nikiwa shuleni nilikuwa nimejifunza Kirusi na nilikuwa nikifanya mazoezi tangu nilipokamatwa. Kwa hiyo, tulipofika kwenye kambi nilikuwa nikizungumza Kirusi vizuri.

      Huko Vorkuta tulikutana na mwanamke kijana kutoka Ukrainia ambaye alijifunza na kuwa Shahidi katika kambi ya mateso ya Nazi huko Poland. Mnamo 1945 yeye na Mashahidi wengine 14 waliingizwa katika meli ambayo Wajerumani walitaka kuizamisha katika Bahari ya Baltiki. Hata hivyo, meli hiyo ilifika salama huko Denmark. Baadaye, aliporudi Urusi, alikamatwa kwa sababu ya kuhubiri na akatumwa huko Vorkuta, ambako alitutia moyo sana.

      Pia tulikutana na wanawake wawili, ambao waliuliza kwa Kiukrainia, “Je, kuna yeyote kati yenu ambaye ni Shahidi wa Yehova?” Mara moja tulitambua kwamba wao ni dada zetu Wakristo! Walitutia moyo na kututunza. Wafungwa wengine walisema ni kana kwamba tulikuwa tukingojewa na washiriki wa familia yetu.

  • Nilijifunza Kumtegemea Mungu
    Amkeni!—2006 | Aprili
    • Katika miaka ya mwishomwisho ya 1950 na katika miaka ya 1960 na ya 1970, Mashahidi waliokuwa wamehamishwa waliendelea kurudi nyumbani. Kufikia mwishoni mwa miaka ya 1980, tulikuwa na Mashahidi zaidi ya 700 nchini Estonia.

  • Nilijifunza Kumtegemea Mungu
    Amkeni!—2006 | Aprili
    • c Hata hivyo, Mashahidi wengi nchini Estonia, walikuwa wamehamishwa mapema mnamo Aprili 1951. Ona Amkeni! la Aprili 22, 2001, ukurasa wa 6-8, na video Faithful Under Trials—Jehovah’s Witnesses in the Soviet Union.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki