-
Mungu na KaisariMnara wa Mlinzi—1996 | Mei 1
-
-
Unyenyekeo Husianifu
14. Nuru iliyoongezeka iliangazwaje kwenye Warumi 13:1, 2 na maandiko yanayohusiana nalo katika 1962?
14 Katika 1961 New World Translation of the Holy Scriptures ilikamilishwa. Utayarishaji wayo ulihitaji uchunguzi wa kina sana wa lugha ya Maandiko. Tafsiri sahihi kabisa ya maneno ambayo hayakutumiwa katika Warumi sura ya 13 pekee bali yaliyotumiwa pia katika mafungu kama Tito 3:1, 2 na 1 Petro 2:13, 17 yalidhihirisha kwamba usemi “mamlaka zilizo kubwa” haukurejezea Mamlaka Kuu Kupita Zote, Yehova, na Mwanaye, Yesu, bali ulirejezea mamlaka za kiserikali za kibinadamu. Mwishoni-mwishoni mwa 1962, makala zilichapishwa katika Mnara wa Mlinzi (Kiingereza) zilizotoa maelezo sahihi ya Warumi sura ya 13 na pia kuandaa mwono wa wazi kuliko ule wa wakati wa C. T. Russell. Makala hizi zilisema kwamba utii wa Kikristo kwa mamlaka hauwezi kuwa kamili. Ni lazima uwe husianifu, ili usifanye watumishi wa Mungu wapingane na sheria za Mungu. Makala zaidi za Mnara wa Mlinzi zimekazia jambo hili muhimu.c
15, 16. (a) Uelewevu mpya wa Warumi sura ya 13 ulitokeza maoni gani yenye usawaziko mzuri zaidi? (b) Ni maswali gani yanayobaki kujibiwa?
15 Ufunguo huu wa uelewevu sahihi wa Warumi sura ya 13 umewezesha watu wa Yehova kusawazisha staha inayostahili mamlaka za kisiasa na msimamo usioridhiana juu ya kanuni za Kimaandiko zilizo muhimu. (Zaburi 97:11; Yeremia 3:15) Umewawezesha wawe na maoni yafaayo juu ya uhusiano wao na Mungu na shughuli zao na Serikali. Umehakikisha kwamba huku wakimpa Kaisari yaliyo ya Kaisari, hawapuuzi kumpa Mungu yaliyo ya Mungu.
-
-
Mungu na KaisariMnara wa Mlinzi—1996 | Mei 1
-
-
Kwa kupendeza, katika kufafanua Warumi sura ya 13, Profesa F. F. Bruce aandika: “Ni wazi katika muktadha wa [Warumi 13], kama ilivyo na muktadha wa ujumla wa maandiko ya kimitume, kwamba serikali yaweza kwa halali kudai utii kutokana tu na viwango vya makusudi ambayo hiyo serikali imewekewa kimungu—hasa, serikali haiwezi kukinzwa tu, bali ni lazima ikinzwe inapodai utii unaopaswa kuwa wa Mungu pekee.”
-