-
Ole wa Kwanza—NzigeUfunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
-
-
“Na wao waliambiwa wasidhuru mmea wowote wa dunia wala kitu chochote cha chanikiwiti wala mti wowote, ila wale watu tu ambao hawana muhuri wa Mungu juu ya vipaji vya nyuso zao.
-
-
Ole wa Kwanza—NzigeUfunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
-
-
10. (a) Tauni hiyo inaelekezwa kwa nani hasa, na kukiwa na tokeo gani kwao? (b) Ni mateso ya namna gani yanayohusika? (Ona pia kielezi cha chini.)
10 Angalia kwamba tauni hii haielekezwi kwanza kwa watu au wale mashuhuri miongoni mwao—ile ‘mimea na miti ya dunia.’ (Linga Ufunuo 8:7.) Nzige wapaswa kudhuru tu wale watu ambao hawana “muhuri wa Mungu juu ya vipaji vya nyuso zao,” wale katika Jumuiya ya Wakristo ambao hudai kuwa wametiwa muhuri lakini rekodi inaonyesha dai hilo kuwa la uwongo. (Waefeso 1:13, 14) Hivyo, matamko yenye kutesa ya nzige wa ki-siku-hizi yalielekezwa kwanza dhidi ya viongozi wa kidini wa Jumuiya ya Wakristo. Ni lazima watu hawa wenye kujitanguliza wawe waliteseka kama nini waliposikia ikitangazwa peupe kwamba hawakuwa wakishindwa tu kuongoza makundi yao yaende mbinguni bali pia wao wenyewe hawangefika huko!d Kwa kweli, kimekuwa kisa cha ‘kipofu akiongoza kipofu’!—Mathayo 15:14.
-