-
Tulipu—Ua Lenye Historia ya FujoAmkeni!—1996 | Julai 8
-
-
Lakini, je, ulijua kwamba tulipu hasa zilianzia Uturuki?
Tulipu za Uholanzi Zenye Asili ya Mashariki
Madoido ya Uturuki ya kuanzia karne ya 12 yaonyesha tulipu, lakini fasihi za Ulaya zataja tulipu kwa mara ya kwanza mnamo miaka ya 1550, asema mtaalamu wa mimea Adélaïde L. Stork. Katika 1553 msafiri mmoja kutoka Ufaransa aliandika kwamba “watu kutoka nchi za kigeni wenye kushangaa” walikuwa wakinunua “lili nyekundu kubwa [zisizo za kawaida]” katika soko za Constantinople (Istanbul). Wenyeji waliita ua hilo dülbend, jina limaanishalo “kilemba” katika Kituruki, na neno hilo, aeleza Dakt. Stork, likawa “chanzo asili cha neno ‘tulipu.’”
Mmoja wa wageni waliovutiwa na maua hayo yenye kufanana na kilemba alikuwa Ogier Ghislain de Busbecq, balozi wa Austria nchini Uturuki (1555-1562). Alichukua baadhi ya tulipu kutoka Constantinople hadi Vienna, ambako zilipandwa katika bustani za Ferdinand 1, maliki wa Hapsburg. Huko tulipu zilisitawi chini ya utunzi stadi wa Charles de L’Écluse—mtaalamu wa mimea Mfaransa aliyejulikana zaidi kwa jina lake la Kilatini, Carolus Clusius.
-
-
Tulipu—Ua Lenye Historia ya FujoAmkeni!—1996 | Julai 8
-
-
Hata hivyo, upendo kwa tulipu uliendelea hata baada ya matokeo ya kichaa cha tulipu, na biashara ya tulipu ikaanza kusitawi tena. Hata kufikia karne ya 18, tulipu za Uholanzi zilikuwa zimekuwa maarufu sana hivi kwamba sultani mmoja wa Uturuki, Ahmed 3, aliingiza nchini mwake maelfu ya tulipu kutoka Uholanzi. Basi baada ya safari ndefu, uzao wa tulipu za Uturuki zilizokuwa Uholanzi ukarudi nchi yao ya awali.
-