Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Uganda
    2010 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
    • Frank na Mary Smith walionyesha roho ya Isaya kwa kuukubali mara moja mwito huo na kuanza kufanya mipango ya kuhamia Afrika Mashariki.a (Isa. 6:8) Julai 1959 waliabiri meli kutoka New York kupitia Cape Town hadi Mombasa. Kisha wakasafiri kwa gari-moshi kwenda Kampala, ambapo Frank alipata kandarasi katika idara ya usoroveya ya serikali. Waliishi Entebbe, kilomita 35 hivi kusini mwa Kampala. Mji huo maridadi ulio kando ya Ziwa Victoria, haukuwa umehubiriwa hata kidogo. Ndugu na Dada Smith walikuwa wakihudhuria mikutano mjini Kampala katika kutaniko dogo lakini lenye ongezeko.

      Muda mfupi baadaye, akina Smith walimhubiria Peter Gyabi, aliyekuwa na cheo katika serikali ya Uganda, pamoja na mke wake, Esther. Awali, Peter alikuwa amepata kitabu What Has Religion Done for Mankind?b lakini hakukisoma kwa makini kwa sababu ya shughuli zake nyingi kazini na kuhamishwa-hamishwa kikazi. Kisha, siku moja Peter alitumwa kutatua mzozo wa shamba kati ya makabila mawili. Alisali, “Mungu, iwapo utanisaidia, nitakutafuta.” Utatuzi ulipopatikana kwa amani, alikumbuka sala yake, naye akaanza kukisoma kile kitabu. Alitambua mambo aliyokuwa akijifunza ni kweli naye akaanza kuwatafuta Mashahidi. Alifurahi sana alipokutana na Frank Smith, aliyekubali kumfundisha yeye na mke wake Biblia kwa ukawaida! Wenzi hao wa ndoa wenye furaha walibatizwa, nao bado ni wahubiri wenye bidii wa Ufalme, zaidi ya miaka 40 baadaye.

  • Uganda
    2010 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
    • a Ripoti kuhusu simulizi la maisha la Ndugu Frank Smith ilichapishwa katika gazeti la Mnara wa Mlinzi la Agosti 1, 1995, ukurasa wa 20-24. Babake Frank, Frank W. Smith, na pia baba yake mdogo na mke wake, Gray na Olga Smith, walikuwa kati ya wahubiri wa kwanza kuhubiri Afrika Mashariki. Babake Frank aliugua malaria na kufa alipokuwa akirudi Cape Town, miezi miwili tu kabla ya Frank kuzaliwa.

  • Uganda
    2010 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
    • [Picha katika ukurasa wa 75]

      Mary na Frank Smith, kabla tu ya kufunga ndoa mwaka wa 1956

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki