Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g99 5/8 uku. 32
  • Kukabiliana na Kifo cha Mtoto Mchanga

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kukabiliana na Kifo cha Mtoto Mchanga
  • Amkeni!—1999
Amkeni!—1999
g99 5/8 uku. 32

Kukabiliana na Kifo cha Mtoto Mchanga

MAMA mmoja kutoka Uingereza aliandika hivi ili kuonyesha uthamini wake kwa ajili ya broshua Mtu Fulani Umpendaye Anapokufa. “Kwa hakika broshua hii ni chakula kwa wakati ufaao kwa familia yetu.” Kisha akaeleza:

“Mambo yaliyoonwa yaliyosimuliwa katika broshua hiyo ni kama yale yaliyotupata. Ilifariji sana kujua kwamba watu wengine wamehisi, na wanaendelea kuhisi kama tulivyohisi.

“Nilithamini hasa ile sehemu iliyoonyesha kwamba kuharibikiwa mimba ni kifo na husababisha huzuni. Kwa sababu mtoto huyo mchanga kwa hakika hajaishi nje ya tumbo la uzazi watu wengi hawamwoni akiwa mtu, na kwa hivyo hawaelewi huzuni inayosababishwa na kifo chake.

“Kuharibika kwa mimba zangu hakukuwa kwa kawaida . . . Nilianzishiwa uchungu wa kuzaa katika pindi zote mbili na nikazaa watoto wafu. Nayarudia maneno ya Veronica (katika ukurasa wa 10 wa broshua hiyo), aliyesema hivi: ‘Kumzaa mtoto mfu ni jambo mbaya sana kwa mama.’”

Labda wewe au mtu fulani unayemjua atapata faraja kwa kusoma broshua hii yenye kurasa 32 inayothaminiwa sana. Unaweza kupokea broshua Mtu Fulani Umpendaye Anapokufa kwa kujaza na kupeleka kuponi iliyopo hapa kwa anwani iliyoonyeshwa au kwa anwani iliyoorodheshwa kwenye ukurasa wa 5 wa gazeti hili.

◻ Nipelekeeni nakala ya broshua Mtu Fulani Umpendaye Anapokufa.

◻ Tafadhali wasilianeni nami kuhusu funzo la Biblia nyumbani bila malipo.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki