-
Nchi Ambazo Zilikuwa Sehemu ya Yugoslavia2009 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
-
-
Nchi Ambazo Zilikuwa Sehemu ya Yugoslavia
ENEO la nchi ambayo hapo zamani iliitwa Yugoslavia lina mambo mbalimbali yenye kuvutia sana. Ulaya ya Kati na Ulaya Mashariki ziko upande wa kaskazini, Ugiriki na Uturuki upande wa kusini, na Italia upande wa magharibi. Eneo hilo lina watu wa utamaduni, lugha, na dini mbalimbali. Hata hivyo, watu wengi wakisikia jina Yugoslavia wanafikiria vita na misukosuko. Tangu kiongozi aliyeitwa Francis Ferdinand alipouawa mwaka wa 1914 mpaka maangamizi ya hivi karibuni ya jamii nzima-nzima, eneo hilo la Rasi ya Balkani limekuwa na migogoro mingi. Watu wa eneo hilo walipopigana ili kupata uhuru walianzisha nchi mbalimbali. Mwishowe, nchi ya Yugoslavia iligawanyika, na sasa katika eneo hilo kuna nchi huru za Bosnia na Herzegovina, Kroatia, Makedonia, Montenegro, Serbia, na Slovenia.
-
-
Nchi Ambazo Zilikuwa Sehemu ya Yugoslavia2009 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
-
-
[Sanduku katika ukurasa wa 144]
Hali Tofauti-Tofauti Katika Ile Iliyokuwa Yugoslavia
Ukiwauliza watu kadhaa wakueleze hali tofauti zilizokuwa katika ile iliyokuwa nchi ya Yugoslavia, inaelekea kwamba utapata majibu mbalimbali. Huenda wote wakakubaliana kwamba kulikuwa na makabila saba yaliyofuata dini tofauti-tofauti na hata yalizungumza lugha tofauti zenye alfabeti tofauti. Kila kabila lina dini yake. Miaka zaidi ya 1,000 iliyopita, dini zinazodai kuwa za Kikristo zilikuwa zimegawanyika katika makundi mawili, dini ya Kikatoliki na dini ya Othodoksi. Nchi iliyoitwa Yugoslavia imegawanyika katikati kabisa kulingana na dini hizo mbili. Watu wengi wanaoishi Kroatia na Slovenia ni Wakatoliki, na wengi wa wale wanaoishi huko Serbia na Makedonia ni Waothodoksi. Nchi ya Bosnia ina mchanganyiko wa Waislamu, Wakatoliki, na Waothodoksi.
Dini imewagawanya watu kama vile lugha zilivyowagawanya. Watu wengi katika ile iliyokuwa Yugoslavia, isipokuwa Kosovo, wanazungumza lugha ya Kislavi ya Kusini. Ingawa kila nchi ina lugha yake, Waserbia, Wakroatia, Wabosnia, na Wamontenegro wanaweza kuwasiliana na kuelewana kwa sababu wanatumia maneno mengi yanayofanana. Lakini hali ni tofauti katika Kosovo, Makedonia, na Slovenia. Mwishoni mwa karne ya 19, jitihada zilifanywa za kuunganisha lugha zinazofanana, lakini nchi ya Yugoslavia iliposambaratika mwaka wa 1991, jitihada hizo zilifikia kikomo. Katika miaka kumi ambayo imepita, nchi zote zimejitahidi sana kuwa tofauti na nchi nyingine kwa kutumia maneno fulani na kuepuka mengine.
-