Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Nchi Ambazo Zilikuwa Sehemu ya Yugoslavia
    2009 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
    • Masimulizi yetu yanaanza na kijana fulani kinyozi anayeitwa Franz Brand, mwenyeji wa eneo la kaskazini la Yugoslavia linaloitwa Vojvodina. Alikuwa ameenda Austria kutafuta kazi. Akiwa huko, alijifunza kweli, kisha akarudi katika mji wao mwaka wa 1925 akiwa Shahidi. Alijiunga na kikundi kidogo ambacho kilikuwa kikisoma na kuzungumzia vitabu vya kujifunzia Biblia vinavyoitwa Studies in the Scriptures, ambavyo walikuwa wamepewa na watu wao wa ukoo walio nchini Marekani.

      Kikundi hicho kilitambua kwamba kinapaswa kuhubiri, na vijitabu viwili vinavyoeleza mafundisho ya Biblia vikatafsiriwa katika Kiserbia. Inahuzunisha kwamba kabla ya vijitabu hivyo kugawanywa, kikundi hicho kilitembelewa na ndugu mwenye madaraka aliyeasi tengenezo na kuanzisha dhehebu lake. Alimshawishi kila mtu aachane na Wanafunzi wa Biblia, lakini alishindwa kumshawishi Franz.

      Franz alihamia Maribor, Slovenia, ambako alipata kazi kwenye saluni ya kunyoa. Alimhubiria mwenye saluni hiyo ya kunyoa, Richard Tautz, akakubali kweli. Franz na Richard waliitwa vinyozi wanaoamini Biblia, na walitumia mahali pao pa kazi kama kituo cha kuhubiri. Watu waliokuja kunyolewa walisikiliza kwa makini sana hivi kwamba hawakutaka kusogea au kuongea walipokuwa wakinyolewa!

  • Nchi Ambazo Zilikuwa Sehemu ya Yugoslavia
    2009 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
    • [Picha katika ukurasa wa 145]

      Franz Brand

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki