-
Nchi Ambazo Zilikuwa Sehemu ya Yugoslavia2009 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
-
-
Mmoja wao alikuwa mwanasiasa, aliyeitwa Ðuro Džamonja. Mwingine aliitwa Rudolf Kalle, na alikuwa na duka la kurekebisha taipureta. Ðuro na Rudolf walifanya maendeleo ya haraka nao wakabatizwa bila kukawia. Ðuro aliacha siasa na kusaidia kuanzisha shirika la The Lighthouse Society of Bible Students katika Ufalme wa Yugoslavia. Shirika hilo la kisheria liliwawezesha akina ndugu kuhubiri na kufanya mikutano kwa uhuru.
-
-
Nchi Ambazo Zilikuwa Sehemu ya Yugoslavia2009 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
-
-
SINEMA YA “PHOTO-DRAMA” ILIFUNGUA NJIA
Mwaka wa 1931, ofisi ya tawi ya Mashahidi wa Yehova katika nchi ya Uswisi ilituma ndugu wawili ili waonyeshe sinema ya “The Photo-Drama of Creation” katika miji yote mikubwa huko Yugoslavia. Majumba yalijaa watu, nao walitazama kwa makini sana Ðuro alipokuwa akionyesha sinema hiyo.
-