Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Nchi Ambazo Zilikuwa Sehemu ya Yugoslavia
    2009 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
    • Upande wa kusini huko Mostar, mji mkuu wa Herzegovina, kiongozi wa kikundi cha wanamuziki anayeitwa Alfred Tuček alitambua kweli naye akawa painia.

  • Nchi Ambazo Zilikuwa Sehemu ya Yugoslavia
    2009 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
    • Kiongozi wa Bendi Anakuwa Painia

      Miaka mingi iliyopita katika nchi inayoitwa leo Bosnia na Herzegovina, kiongozi wa Bendi ya Royal Guards, Alfred Tuček, alipewa vichapo vinavyozungumzia Biblia na mfanyakazi mwenzake Fritz Gröger. Alfred aliwasiliana na shirika la Lighthouse Society labda mwishoni mwa miaka ya 1920, huko Maribor, akasema kwamba alitaka kuwa painia wa kawaida. Muda si muda, akawa kati ya mapainia wa kwanza nchini Yugoslavia. Hata ingawa alikuwa na kazi yenye mshahara mnono akiwa kiongozi wa bendi ya jeshi, upendo wake kwa Yehova ulimsukuma aache kazi hiyo na akaamua ‘kutotazama mambo yaliyo nyuma.’ (Luka 9:62) Mwanzoni mwa miaka ya 1930, alisafiri pamoja na ndugu mapainia kutoka Ujerumani na kuwaonyesha watu sinema ya “Photo-Drama of Creation.” Pia, alisaidia sana kuchora ramani za maeneo na kupanga kazi ya kuhubiri nchini Yugoslavia. Mwaka wa 1934, alimwoa Frida, mmoja wa mapainia waliotoka Ujerumani. Mgawo wao wa kwanza ulikuwa Sarajevo, Bosnia. Baadaye, walihubiri habari njema katika sehemu fulani za Makedonia, Montenegro, Kroatia, na Serbia. Mwanzoni walisafiri sana kwa baiskeli, lakini baadaye walitumia pikipiki. Ingawa watu hawakukubali habari njema mara moja wakati huo na kwamba kazi ya kuhubiri ilikuwa imepigwa marufuku, walitambua umuhimu wa kuwahubiria watu wengi iwezekanavyo.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki