-
Young People Ask—What Will I Do With My Life? (Sehemu ya 1)Huduma ya Ufalme—2012 | Septemba
-
-
Young People Ask—What Will I Do With My Life? (Sehemu ya 1)
Vijana wanapokua kuelekea utu uzima, wanapaswa kufanya maamuzi muhimu. Ili kuwasaidia, video Young People Ask—What Will I Do With My Life? imetayarishwa. Katika menu kuu, chagua Play Drama, kisha jaribu kujibu maswali yaliyo katika fungu la 2. Halafu, chagua Interviews kwenye menu kuu, kisha uchague Looking Back, na ujaribu kujibu maswali yaliyo katika fungu la 3.
Drama: (1) Ni katika njia zipi hali ya Timotheo inafanana na hali ya vijana wengi Wakristo leo? (2) Andre alishinikizwa jinsi gani afanye vizuri zaidi katika riadha? (3) Ndugu Fleissig alimwambia nini Andre kuhusu (a) kujitoa kwa Yehova na kujitoa kwa ajili ya mchezo fulani? (Mt. 6:24) (b) chanzo cha furaha ya kweli? (c) kile ambacho alikumbuka kutokana na bakuli yake aliyopata katika kambi ya mateso? (d) watu aliopigwa nao picha pamoja na mke wake? (e) ikiwa alijuta kuacha malengo aliyokuwa nayo? (Flp. 3:8) (4) Nyanya ya Andre alijibuje swali aliloulizwa na Andre, “Je, ni vibaya nikitaka kuwa bingwa wa riadha?” (Luka 4:5-7) (5) Je, kushinda katika riadha kulimletea Andre uradhi wa kweli? (6) Ni jambo gani lililokuvutia katika barua ya mwisho ya Ndugu Fleissig aliyomwandikia Andre? (Met. 10:22) (7) Ndugu Fleissig alimsaidia Andre kugundua nini?
Kufikiria Mambo Yaliyopita (Looking Back): (8) Ndugu na dada walioonyeshwa katika sehemu hii walikuwa wakifuatilia kazi gani, na kwa nini? (9) Walipata mafanikio gani? (10) Ni nini kilichowafanya wabadili maisha yao? (2 Kor. 5:15) (11) Wamejitahidi kufikia miradi gani ya kitheokrasi badala ya kazi walizokuwa nazo, na ni kwa nini waliona hawawezi kufuatilia miradi yote miwili? (12) Je, walijuta kwa sababu ya kubadili mambo waliyokazia maishani? (13) Walisema jambo gani ambalo limekufanya ufikiri kuhusu jinsi utakavyoyatumia maisha yako?
Tafadhali tazama mahojiano hayo mengine pamoja na habari ya ziada, na ujitayarishe kutoa maelezo kuzihusu zinapozungumziwa katika Mkutano wa Utumishi juma lijalo.
-
-
Young People Ask—What Will I Do With My Life? (Sehemu ya 2)Huduma ya Ufalme—2012 | Septemba
-
-
Young People Ask—What Will I Do With My Life? (Sehemu ya 2)
Kwenye menu kuu ya video Young People Ask—What Will I Do With My Life? chagua Interviews, kisha chagua Sections. Baada ya kutazama kila moja ya sehemu hizo tatu, tumia maswali yaliyo katika fungu la 2 ili kupitia habari hiyo. Kisha kwenye menu kuu chagua Supplementary Material na baada ya kutazama kila moja ya mahojiano hayo matano ya ziada, tumia maswali yaliyo katika fungu la 3 ili kupitia habari hiyo.
Visehemu (Sections)—Kujitoa kwa Mambo Yasiyo ya Maana au kwa Mungu (Dedication to Vain Pursuits or to God): (1) Ni miradi gani ambayo vijana hushinikizwa kuifuatilia? (2) Andiko la 1 Yohana 2:17 linawezaje kuwasaidia vijana kuamua kiasi cha elimu ambacho watafuatilia? (3) Kwa nini hatupaswi kuruhusu woga utuzuie kubatizwa? (4) Ni baadhi ya mambo gani ambayo yataweza kutusaidia kufikia hatua ya ubatizo? Kujifunza Kufurahia Huduma Yako (Learning to Enjoy Your Ministry): (5) Kwa nini wengine hawafurahii huduma? (6) Ni baadhi ya mambo gani yanayoweza kutusaidia? (7) Ni nini ambacho wengine huogopa zaidi kuliko kuzungumza na mtu wasiyemfahamu, na kwa nini? (8) Tunawezaje kushinda woga wetu na kukuza ujasiri wa kuzungumza? (9) Kwa nini ni muhimu pia kusitawisha kiwango fulani cha ustadi katika huduma? Mlango Ulio Wazi wa Utumishi (An Open Door to Service): (10) Upainia hutoaje fursa nyingi za kufanya maendeleo kiroho? (Flp. 3:16) (11) Kwa nini wengine husita kuanza upainia? (12) Ni kanuni gani za Kimaandiko zinazoweza kutusaidia kushinda mahangaiko ya kiuchumi? (13) Wengine wamefanya nini ili kujitegemeza kifedha huku wakifanya upainia? (14) Mtu anaweza kufanya nini iwapo hali hazimruhusu kuanza utumishi wa wakati wote?
Habari ya Ziada (Supplementary Material)—Thamani ya Funzo la Kibinafsi (The Value of Personal Study): (15) Kwa nini ni muhimu kuwa na mazoea mazuri ya kujifunza kibinafsi? Mahubiri ya Badala (Alternative Witnessing) (ambayo sasa yanaitwa mahubiri ya hadharani): (16) Kushiriki katika aina mbalimbali za huduma kutaongezaje shangwe yetu? Utumishi wa Betheli (Bethel Service): (17) Ni zipi baadhi ya shangwe za utumishi wa Betheli? Shule ya Mazoezi ya Kihuduma (Ministerial Training School): (18) Wale ambao wamehudhuria shule hiyo (ambayo sasa inaitwa Shule ya Biblia ya Ndugu Waseja) wamefaidikaje? Shule ya Wamishonari ya Gileadi (Gilead Missionary Training): (19) Peter na Fiona walijitayarishaje kwa ajili ya utumishi wa umishonari, nao walinufaikaje kutokana na shule ya Gileadi?
-