Young People Ask—What Will I Do With My Life? (Sehemu ya 1)
Vijana wanapokua kuelekea utu uzima, wanapaswa kufanya maamuzi muhimu. Ili kuwasaidia, video Young People Ask—What Will I Do With My Life? imetayarishwa. Katika menu kuu, chagua Play Drama, kisha jaribu kujibu maswali yaliyo katika fungu la 2. Halafu, chagua Interviews kwenye menu kuu, kisha uchague Looking Back, na ujaribu kujibu maswali yaliyo katika fungu la 3.
Drama: (1) Ni katika njia zipi hali ya Timotheo inafanana na hali ya vijana wengi Wakristo leo? (2) Andre alishinikizwa jinsi gani afanye vizuri zaidi katika riadha? (3) Ndugu Fleissig alimwambia nini Andre kuhusu (a) kujitoa kwa Yehova na kujitoa kwa ajili ya mchezo fulani? (Mt. 6:24) (b) chanzo cha furaha ya kweli? (c) kile ambacho alikumbuka kutokana na bakuli yake aliyopata katika kambi ya mateso? (d) watu aliopigwa nao picha pamoja na mke wake? (e) ikiwa alijuta kuacha malengo aliyokuwa nayo? (Flp. 3:8) (4) Nyanya ya Andre alijibuje swali aliloulizwa na Andre, “Je, ni vibaya nikitaka kuwa bingwa wa riadha?” (Luka 4:5-7) (5) Je, kushinda katika riadha kulimletea Andre uradhi wa kweli? (6) Ni jambo gani lililokuvutia katika barua ya mwisho ya Ndugu Fleissig aliyomwandikia Andre? (Met. 10:22) (7) Ndugu Fleissig alimsaidia Andre kugundua nini?
Kufikiria Mambo Yaliyopita (Looking Back): (8) Ndugu na dada walioonyeshwa katika sehemu hii walikuwa wakifuatilia kazi gani, na kwa nini? (9) Walipata mafanikio gani? (10) Ni nini kilichowafanya wabadili maisha yao? (2 Kor. 5:15) (11) Wamejitahidi kufikia miradi gani ya kitheokrasi badala ya kazi walizokuwa nazo, na ni kwa nini waliona hawawezi kufuatilia miradi yote miwili? (12) Je, walijuta kwa sababu ya kubadili mambo waliyokazia maishani? (13) Walisema jambo gani ambalo limekufanya ufikiri kuhusu jinsi utakavyoyatumia maisha yako?
Tafadhali tazama mahojiano hayo mengine pamoja na habari ya ziada, na ujitayarishe kutoa maelezo kuzihusu zinapozungumziwa katika Mkutano wa Utumishi juma lijalo.