-
Watartari—Maisha Yao ya Kale, Sasa, na Wakati UjaoAmkeni!—2011 | Septemba
-
-
Kazan’ ni jiji la kisasa lenye wakazi milioni moja mahali ambapo Mto Volga na Mto Kazanka hukutania. Ni moja kati ya majiji mengi nchini Urusi yaliyo na mifumo ya reli za chini ya ardhi.c Kila kituo kimetengenezwa kwa njia ya pekee. Vingine vina muundo wa kisasa na vingine vimejengwa kwa njia inayoonyesha utamaduni wa watu wa nchi za Mashariki, ilhali vingine vimejengwa kwa njia inayoonyesha utamaduni wa Enzi za Kati. Kituo kimoja mjini Kazan’ kimepambwa kwa michoro 22 maridadi iliyotiwa nakshi inayoonyesha hekaya za kitamaduni za Watartari.
Chuo Kikuu cha Kitaifa cha Kazan kilianzishwa mwaka wa 1804 na aliyekuwa Maliki wa Urusi Alexander wa Kwanza na kina moja ya maktaba kubwa zaidi nchini Urusi. Chuo hicho kina uvutano mkubwa kwani ni kituo cha elimu na tamaduni na ndicho kilichochangia kusitawi kwa vyuo vingine huko Tatarstan. Kati ya vichapo 5,000,000 vinavyopatikana humo mna hati 30,000 za zamani, ambazo baadhi yake ni za tangu karne ya tisa W.K.
Inafurahisha kutembea kwenye Barabara ya Bauman katikati mwa jiji. Eneo hilo limejaa maduka na mikahawa yenye kupendeza. Tulipotembelea eneo hilo hivi karibuni, mimi na mke wangu tulifurahia kupanda mashua kwenye Mto Volga baada ya kutalii mji huo.
Sehemu moja yenye kupendeza katika mji wa Kazan’ ni ngome maarufu ya kremlin. Ngome hiyo ya zamani, yenye majengo ya tangu karne ya 16, ndiyo ngome pekee ya Kitartari ambayo imedumu hadi leo nchini Urusi. Kwenye ukingo wa ukuta wa mawe wa Kremlin hiyo ya Kazan’ utaona Mnara wa Syuyumbeki, majengo ya serikali ya Tatarstan, msikiti, na kanisa la Othodoksi.
Katika mwaka wa 2000, Kremlin hiyo ya Kazan’ ilichaguliwa kuwa Eneo Linalostahili Kuhifadhiwa Ulimwenguni la UNESCO. Wakati wa usiku jengo la kremlin hupendeza sana. Hiyo ni kwa sababu ya taa zake zinazomulika na kung’aa mtoni.
-
-
Watartari—Maisha Yao ya Kale, Sasa, na Wakati UjaoAmkeni!—2011 | Septemba
-
-
[Picha katika ukurasa wa 25]
Kremlin ya Kazan’ katika Mto Kazanka
[Hisani]
© Michel Setboun/CORBIS
-