-
Makaburi Hutufunulia Imani za KaleAmkeni!—2005 | Desemba 8
-
-
Maisha ya Baadaye ya Wamisri
Piramidi za Misri karibu na Cairo na vyumba vya kuzikia watu katika Bonde la Wafalme karibu na Luxor ni miongoni mwa makaburi maarufu zaidi kati ya makaburi yote ya kale. Neno ambalo Wamisri wa kale walitumia kwa “kaburi” lilimaanisha pia “nyumba”—per. “Kwa hiyo, mtu alikuwa na nyumba wakati alipokuwa hai na baada ya kufa,” asema Christine El Mahdy katika kitabu chake Mummies, Myth and Magic in Ancient Egypt. Pia anasema kwamba “kulingana na imani [ya Wamisri], ilikuwa lazima mwili uendelee kuishi ili sehemu nyingine, yaani, ka, ba, na akh pia ziendelee kuwa hai.”
Ka ilikuwa nakala ya kiroho ya mwili nayo ilitia ndani matarajio, tamaa, na mahitaji yake. Baada ya kifo, ka ilitengana na mwili na kuishi kaburini. Kwa kuwa ka ilihitaji kila kitu ambacho mtu alihitaji maishani, “vitu vilivyowekwa kaburini viliwekwa hapo hasa ili kutosheleza mahitaji ya ka,” aandika El Mahdy. Ba inaweza kulinganishwa na sifa za mtu au utu, nayo iliwakilishwa na ndege mwenye kichwa cha binadamu. Ba iliingia mwilini mtu alipozaliwa na kutengana na mwili wakati wa kifo. Sehemu ya tatu, yaani, Akh, “iliibuka” kutoka kwenye mwili uliotiwa mumiani wakati maneno ya kichawi yalipokuwa yakitamkwa.a Akh iliishi katika ulimwengu wa miungu.
Kwa kugawanya mwanadamu katika sehemu tatu, Wamisri walipiga hatua moja zaidi kuliko wanafalsafa Wagiriki wa kale ambao waligawanya mwili wa binadamu katika sehemu mbili, yaani, mwili na “nafsi” yenye ufahamu. Ingawa fundisho hilo lingali linapendwa, haliungwi mkono na Biblia ambayo inasema: “Walio hai wanajua kwamba watakufa; lakini wafu, hawajui lolote kamwe.”—Mhubiri 9:5.
-
-
Makaburi Hutufunulia Imani za KaleAmkeni!—2005 | Desemba 8
-
-
[Hisani ya Picha katika ukurasa wa 23]
Kushoto: Kifuniko cha mazishi cha dhahabu cha Mfalme Tutankhameni wa Misri; chini: Mchoro wa “ba” kwenye kaburi, akiwa kama ndege mwenye kichwa cha binadamu
-