Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • “Mimi Niko Tayari Kwenda”
    Mnara wa Mlinzi (Toleo la Watu wote)—2016 | Na. 3
    • Jioni moja baada ya kujaza mtungi wake, mwanaume mzee alimkimbilia. Akamwambia hivi: “Tafadhali, nipe maji kidogo katika mtungi wako.” Mtu huyo alitoa ombi hilo kwa upole sana! Rebeka aliona kuwa mwanaume huyo alikuwa amesafiri kutoka mbali sana. Hivyo akashusha mtungi wake begani na kumpa mwanaume huyo maji baridi yenye kuburudisha. Pia alitambua kwamba mwanamume huyo alikuwa na ngamia kumi waliopiga magoti karibu na chombo cha kunyweshea wanyama ambacho hakikuwa kimejazwa maji. Isitoshe, Rebeka alitaka kumwonyesha ukarimu mwanamume huyo kadiri alivyoweza. Hivyo, akamwambia: “Nitateka maji pia kwa ajili ya ngamia zako mpaka wamalize kunywa.”—Mwanzo 24:17-19.

      Ona kwamba Rebeka hakujitolea tu kuwapa ngamia kumi maji kidogo ya kunywa, bali alitaka kuwapa maji mengi hadi watakapotosheka. Ngamia mmoja mwenye kiu sana anaweza kunywa zaidi ya lita 95 za maji! Ikiwa ngamia wote kumi walikuwa na kiu sana, basi Rebeka alifanya kazi hiyo ngumu kwa saa nyingi. Hata hivyo, inaonekana ngamia hao hawakuwa na kiu sana.a Je, Rebeka alijua jambo hilo alipojitolea kuwapa maji? Hapana. Alikuwa tayari, hata alikuwa na hamu ya kufanya kazi kwa bidii sana ili kumwonyesha ukarimu mzee huyo mgeni. Mwanamume huyo alikubali msaada wake. Kisha alimtazama kwa makini kila mara alipokuwa akifanya kazi ya kwenda na kurudi ili kujaza mtungi wake na kumimina maji katika chombo cha kunyweshea wanyama.—Mwanzo 24:20, 21.

      Rebeka akiwanywesha maji ngamia wa mtumishi wa Abrahamu

      Rebeka alikuwa mwenye bidii na mkarimu

  • “Mimi Niko Tayari Kwenda”
    Mnara wa Mlinzi (Toleo la Watu wote)—2016 | Na. 3
    • a Tayari ilikuwa jioni. Simulizi halitaji kwamba Rebeka alibaki kisimani kwa saa nyingi. Halionyeshi kwamba familia yake ilikuwa imelala usingizi alipomaliza kuchota maji au kama kuna mtu yeyote aliyemtafuta kwa sababu alichelewa kurudi.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki