Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • “Ninawezaje Kufanya Ubaya Huu Mkubwa?”
    Mnara wa Mlinzi—2014 | Novemba 1
    • Katika kisa cha Yosefu, hali ilikuwa mbaya zaidi. Mke wa Potifa alitaka kulipa kisasi. Mara moja akaanza kupiga kelele, na kuwaita watumishi wengine wa nyumba yake. Akawaambia kwamba Yosefu alitaka kumbaka lakini akakimbia alipolia kwa sauti kubwa. Akaliweka vazi lake kando yake mpaka mume wake aliporudi. Potifa aliporudi nyumbani, akamwambia maneno hayohayo, na kudai kuwa lilikuwa kosa la mume wake kumleta mtumishi huyo nyumbani kwao. Potifa alifanya nini? Tunasoma hivi: “Hasira yake ikawaka”! Akamfunga gerezani.—Mwanzo 39:13-20.

      “WAKAITESA MIGUU YAKE KWA PINGU”

      Hatujui mengi kuhusu magereza ya Misri yalivyokuwa wakati huo. Wachimbuaji wa vitu vya kale walipata magofu ya maeneo hayo—ngome kubwa iliyokuwa na vyumba vya magereza na mapango. Baadaye Yosefu alifafanua eneo hilo kwa neno ambalo kihalisi lilimaanisha “tundu,” ambalo linatoa wazo la eneo lisilo na mwanga wala tumaini lolote. (Mwanzo 40:15) Katika kitabu cha Zaburi, tunajifunza kwamba Yosefu alikuwa akiteseka: “Wakaitesa miguu yake kwa pingu, Nafsi yake ikaingia katika vyuma.” (Zaburi 105:17, 18) Wakati mwingine Wamisri waliweka mikono ya wafungwa mgongoni na kuifunga kwa pingu kwenye viwiko; wengine walifungwa kola za chuma shingoni. Lazima Yosefu awe aliumia sana kwa kutendewa isivyofaa—kwa kuwa hakuwa amefanya kosa lolote!

      Isitoshe, hali hiyo iliendelea kwa muda mrefu. Simulizi hilo linasema kwamba Yosefu “akaendelea kuwa humo katika nyumba ya gereza.” Alikaa kwa miaka mingi mahali hapo penye mateso!a Pia, Yosefu hakujua kama angeachiliwa. Hali hizo zenye kutisha zilipoendelea kwa majuma kadhaa, kisha miezi, Yosefu aliwezaje kuvumilia bila kupoteza tumaini au kukata tamaa?

  • “Ninawezaje Kufanya Ubaya Huu Mkubwa?”
    Mnara wa Mlinzi—2014 | Novemba 1
    • a Biblia inaonyesha kwamba Yosefu alikuwa na umri wa miaka 17 au 18 alipoingia katika nyumba ya Potifa na alikaa huko kwa muda mrefu vya kutosha kukua kufikia kuwa mwanamume—huenda miaka kadhaa. Alikuwa na umri wa miaka 30 alipoachiliwa kutoka gerezani.—Mwanzo 37:2; 39:6; 41:46.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki