-
Macho Yako Yanamtazama Nani?Mnara wa Mlinzi (Funzo)—2018 | Julai
-
-
5-7. Ni tatizo gani lililozuka muda mfupi baada ya Waisraeli kutoka Misri, na Musa alilishughulikiaje?
5 Katika kipindi kisichozidi miezi miwili tangu Waisraeli walipotoka Misri—hata kabla hawajafika kwenye Mlima Sinai—tatizo fulani kubwa lilitokea. Watu walianza kulalamika kwamba hakukuwa na maji. Walianza kumnung’unikia Musa, na hali ilizidi kuwa mbaya hivi kwamba Musa akamlilia Yehova akisema: “Nifanye nini na watu hawa? Hivi punde watanipiga mawe!” (Kut. 17:4) Yehova alimjibu Musa kwa kumpa maagizo yaliyo wazi. Alipaswa kuchukua fimbo yake na kuupiga mwamba huko Horebu, na baada ya hapo maji yangebubujika. Tunasoma hivi: “Musa akafanya hivyo mbele ya wazee wa Israeli.” Waisraeli walikunywa maji na kutosheka, na hivyo tatizo hilo likasuluhishwa.—Kut. 17:5, 6.
-
-
Macho Yako Yanamtazama Nani?Mnara wa Mlinzi (Funzo)—2018 | Julai
-
-
11. Kwa nini huenda Musa alipoupiga mwamba Waisraeli wangefikiri kwamba huo haukuwa muujiza wa Yehova?
11 Kuna uwezekano mwingine. Miamba iliyo karibu na eneo la Meriba ya kwanza ilikuwa imefanyizwa na mawe magumu ya matale au graniti. Mwamba wa graniti hauwezi kwa vyovyote kutoa maji hata upigwe kwa nguvu kadiri gani. Hata hivyo, miamba iliyo katika eneo la Meriba ya pili ni tofauti kabisa, na mara nyingi ni ya chokaa nyepesi. Kwa sababu chokaa huwa na matundu-matundu, mara nyingi maeneo yenye miamba ya chokaa huwa na maji chini ya ardhi, hivyo mtu anaweza kuchimba na kupata maji. Je, inawezekana kwamba Musa alipoupiga mwamba huo mara mbili, aliwapa watu sababu ya kufikiri kwamba maji yalitokea tu yenyewe kiasili na si Yehova aliyeyatokeza? Musa alipoupiga mwamba badala ya kuzungumza nao, je, aliwafanya watu waone kana kwamba huo haukuwa muujiza?b Hatuwezi kuwa na uhakika kuhusu hilo.
-