Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Hekima ya Kuishi Katika Ulimwengu Wenye Kutatanisha
    Amkeni!—2002 | Novemba 22
    • Biblia inatusaidia kuelewa suala hili zito kwa kutueleza maoni ya Mungu kuhusu watoto wasiozaliwa bado. Katika Israeli la kale, Mungu alimwona mtu aliyemjeruhi mwanamke mjamzito au mtoto wake asiyezaliwa bado, kuwa muuaji. Alitozwa “uhai kwa uhai.”a (Kutoka 21:22, 23) Kwa hiyo, tunaweza kusema kwa uhakika kwamba Muumba anaona uhai wa kila mwanadamu kuwa mtakatifu, hata uhai wa mtoto asiyezaliwa bado. Kwa kweli, Mungu hupendezwa nasi tunapokuwa tungali tumboni, kama mtunga-zaburi anavyofunua: “Macho yako yaliniona kabla sijakamilika; chuoni mwako ziliandikwa zote pia.”—Zaburi 139:16.

  • Hekima ya Kuishi Katika Ulimwengu Wenye Kutatanisha
    Amkeni!—2002 | Novemba 22
    • a Watu fulani wamedai kwamba sheria hii ilihusu kumjeruhi mama peke yake. Hata hivyo, maandishi ya awali ya Kiebrania hayasemi hivyo. Wasomi wa Biblia wenye kuheshimiwa C. F. Keil na F. Delitzsch wanasema kwamba kulingana na maandishi ya Kiebrania, “yaonekana maneno hayo hayahusu kamwe kumjeruhi mwanamke peke yake.”—Ona Mnara wa Mlinzi, Agosti 1, 1977, Kiingereza, ukurasa wa 478.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki