-
Kutoka kwa Utumwa wa Kutengeneza Matufali Kwenda Kwenye Uhuru!Mnara wa Mlinzi—1987 | Novemba 15
-
-
Waebrania waliokaribishwa katika Misri wakati wa Yusufu walibarikiwa na Mungu kwa ongezeko, wakiwaogopesha sana Wamisri. Tunasoma hivi: “Basi wakaweka wasimamizi juu [ya Waebrania] wawatese kwa mizigo yao. Nao wakamjengea Farao miji . . . Wamisri wakawatumikisha wana wa Israeli kwa ukali; wakafanya maisha yao kuwa uchungu kwa kazi ngumu; kazi ya chokaa na ya matufali.”—Kutoka 1; 7-14.
Upande wa kulia, unaweza kuona kwamba matufali yangali yakitengenezwa katika Misri, mengine yayo yakikaushwa katika majoko kama lile unaloona hapa. (Linganisha Mwanzo 11:1-3; 19:28.) Hata hivyo, kwa wazi, matufali yaliyo mengi ya Wamisri wa kale yalikaushwa kwa jua. Jambo linaloendelea ni matumizi ya majani makavu katika kutengeneza matufali. Majani makavu yanaonekana katika matufali yanayopatikana katika magofu yaliyochimbuliwa ya Beersheba wa kale (picha ndogo imeonyeshwa).
Kuongeza majani makavu kulifanya matufali yawe yenye nguvu. Ili kuyatengeneza, matope (au udongo), maji, na majani makavu yalikanyagwa-kanyagwa pole pole kwa miguu, kisha yakashindiliwa katika kalibu, na mwishowe yanawekwa nje ili yakauke. Ebu wazia ukifanya kazi ngumu kama hiyo siku moja baada ya nyingine. Kwa kweli, unaweza kufahamu kwa nini Waisraeli ‘waliugua kwa sababu ya ule utumwa, wakalia; kilio chao kikafika juu kwa Mungu kwa sababu ya ule utumwa.’—Kutoka 2:23.
Yehova aliwasikia naye akampeleka Musa kwa Farao ili Waisraeli wapate uhuru. Badala ya hilo, Farao mwenye kiburi aliongeza mzigo wao. Sasa iliwapasa wakusanye majani yao makavu wenyewe na bado watengeneze kiasi kile kile cha matufali kama walivyofanya mmwanzoni. Kwani, huku kulikuwa kama kuhukumiwa kifo! Mungu akasema: “Sasa utaona nitakavyomtenda Farao; maana kwa mkono hodari atawapa ruhusu kwenda zao.”—Kutoka 5:1–6:1.
-
-
Kutoka kwa Utumwa wa Kutengeneza Matufali Kwenda Kwenye Uhuru!Mnara wa Mlinzi—1987 | Novemba 15
-
-
[Picha ya ukurasa mzima katika ukurasa wa 31]
[Picha Credit Line katika ukurasa wa 2]
Photos, pages 30, 31: Pictorial Archive (Near Eastern History) Est.
-