-
Tii kwa Uaminifu Mamlaka ya KimunguMnara wa Mlinzi—2002 | Agosti 1
-
-
13. (a) Kwa nini waasi hao walionyesha kimbelembele kwa kufukiza uvumba mbele za Yehova? (b) Yehova aliwatendeaje waasi hao?
13 Kulingana na Sheria ya Mungu, makuhani peke yao ndio waliopaswa kufukiza uvumba. Waasi hao walipaswa kushtuka kwa kukumbuka kwamba Mlawi asiye kuhani hapaswi kufukiza uvumba mbele za Yehova. (Kutoka 30:7; Hesabu 4:16) Kora na watu waliokuwa wakimwunga mkono hawakushtuka! Siku iliyofuata ‘alikutanisha mkutano wote kinyume chao Musa na Aroni mlangoni pa hema ya kukutania.’ Simulizi hilo linatuambia: “Kisha BWANA akanena na Musa na Haruni, na kuwaambia, Jitengeni ninyi mkaondoke kati ya mkutano huu, ili nipate kuwaangamiza mara moja.” Lakini Musa na Aroni walimsihi Yehova asiangamize mkutano huo. Yehova alisikiliza maombi yao. Lakini kuhusu Kora na watu waliomwunga mkono, ‘moto ulitoka kwa BWANA, ukawateketeza hao watu mia mbili hamsini waliofukiza uvumba.’—Hesabu 16:19-22, 35.c
-
-
Tii kwa Uaminifu Mamlaka ya KimunguMnara wa Mlinzi—2002 | Agosti 1
-
-
c Nyakati za wazee wa ukoo, kila kichwa cha familia aliwakilisha mke na watoto wake mbele za Mungu, na hata kutoa dhabihu kwa niaba yao. (Mwanzo 8:20; 46:1; Ayubu 1:5) Hata hivyo, Sheria ilipotolewa, Yehova alichagua wanaume kutoka familia ya Aroni kuwa makuhani ambao wangewatolea watu dhabihu. Yaonekana waasi hao 250 hawakutaka kukubali badiliko lililofanywa katika mpango huo.
-