-
Alitenda kwa BusaraIgeni Imani Yao
-
-
9, 10. (a) Daudi na wanaume wake walipambana na hali gani? (b) Kwa nini Nabali alipaswa kuthamini kile alichofanyiwa na Daudi na watumishi wake? (Ona pia maelezo ya chini kwenye fungu la 10.)
9 Nabali aliishi huko Maoni lakini alifanya kazi katika mji wa Karmeli uliokuwa karibu ambako inaelekea alikuwa na shamba.a Miji hiyo ilikuwa kwenye maeneo yaliyoinuka yenye nyasi, mahali palipofaa kwa ufugaji wa kondoo, na Nabali alikuwa na kondoo 3,000. Hata hivyo, maeneo yote ya kandokando yalikuwa mbuga. Upande wa kusini kulikuwa na nyika kubwa ya Parani. Upande wa mashariki, kulikuwa na mwingilio wa Bahari ya Chumvi uliokuwa na maeneo makavu yenye mabonde na mapango. Katika maeneo hayo, Daudi na wanaume wake walipambana ili kuishi, na bila shaka waliwinda wanyama ili kupata chakula huku wakivumilia hali ngumu. Mara nyingi, walikutana na vijana wachungaji ambao walikuwa wafanyakazi wa tajiri Nabali.
-
-
Alitenda kwa BusaraIgeni Imani Yao
-
-
a Huo haukuwa Mlima maarufu wa Karmeli uliokuwa mbali upande wa kaskazini ambako baadaye nabii Eliya alikabiliana na manabii wa Baali. (Ona Sura ya 10.) Mji huo wa Karmeli ulikuwa kando ya nyika ya kusini.
-