Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Alitenda kwa Busara
    Igeni Imani Yao
    • Abigaili Mrembo

      SURA YA TISA

      Alitenda kwa Busara

      1-3. (a) Ni mambo gani yaliyofanya Abigaili na nyumba yake wakabili hatari? (b) Tutajifunza nini kumhusu mwanamke huyu mwenye sifa za pekee?

      ABIGAILI aliona kwamba kijana aliyekuja kumwona alikuwa ameshtuka sana. Kijana huyo alikuwa na sababu nzuri ya kushtuka. Kulikuwa na hatari. Wakati huo, wapiganaji 400 hivi walikuwa njiani, wakiwa wameazimia kumuua kila mwanamume katika nyumba ya Nabali, mume wa Abigaili. Kwa nini?

      2 Nabali ndiye aliyesababisha hali hiyo. Kama kawaida, alikuwa ametenda kwa ukatili na ukaidi. Hata hivyo, wakati huu alikuwa amekosea sana, alikuwa amemtukana kamanda wa kikundi cha wapiganaji washikamanifu waliozoezwa vizuri. Sasa, mfanyakazi kijana wa Nabali, labda mchungaji, alienda kumwona Abigaili, akitumaini kwamba angefikiria mbinu ya kuwaokoa. Lakini mwanamke mmoja angezuiaje jeshi hilo?

      Mwanamke mmoja angezuiaje jeshi hilo?

  • Alitenda kwa Busara
    Igeni Imani Yao
    • “Akawakemea kwa Sauti Kali”

      8. Nabali alikuwa amemtukana nani, na kwa nini tunaweza kusema hilo lilikuwa tendo lisilo la hekima kabisa?

      8 Nabali alikuwa amefanya hali ya Abigaili kuwa ngumu hata zaidi. Nabali alikuwa amemtukana Daudi. Daudi alikuwa mtumishi mwaminifu wa Yehova ambaye alitiwa mafuta na nabii Samweli, kuonyesha kwamba alikuwa amechaguliwa na Mungu awe mfalme baada ya Sauli. (1 Sam. 16:1, 2, 11-13) Daudi alikuwa akimkimbia Mfalme Sauli muuaji na mwenye wivu, na alikuwa akiishi jangwani pamoja na wapiganaji wake 600 washikamanifu.

  • Alitenda kwa Busara
    Igeni Imani Yao
    • 12 Alikasirika sana! “Akawakemea kwa sauti kali,” hivyo ndivyo yule kijana aliyetajwa mwanzoni alivyomweleza Abigaili tukio hilo. Nabali mwenye uchoyo alilalamika kwa sauti kubwa kuhusu maji, nyama, na mkate wake wenye thamani. Alimdhihaki Daudi kuwa mtu asiye wa maana na akamlinganisha na mtumishi aliyetoroka. Huenda Nabali alikuwa na maoni kama ya Sauli, ambaye alimchukia Daudi. Nabali na Sauli hawakuwa na maoni ya Yehova. Mungu alimpenda Daudi na hakumwona kuwa mtumwa mwasi, bali mfalme wa wakati ujao wa Israeli.​—1 Sam. 25:10, 11, 14.

  • Alitenda kwa Busara
    Igeni Imani Yao
    • 14. (a) Abigaili alichukuaje hatua ya kwanza ili kurekebisha kosa la Nabali? (b) Tunaweza kujifunza nini kutokana na tofauti kati ya mtazamo wa Nabali na Abigaili? (Ona pia maelezo ya chini.)

      14 Kwa njia fulani, tayari tumemwona Abigaili akichukua hatua ili kurekebisha kosa hilo baya. Alikuwa tayari kusikiliza, tofauti na Nabali mume wake. Yule mtumishi kijana alisema hivi kumhusu Nabali: “Yeye ni mtu asiyefaa kitu sana hata mtu hawezi kusema naye.”c (1 Sam. 25:17) Inasikitisha kwamba Nabali hakutaka kusikiliza kwa sababu alijiona kuwa mtu wa maana sana. Leo, watu wengi wana kiburi kama hicho. Lakini yule kijana alijua kwamba Abigaili alikuwa tofauti, na hiyo ndiyo sababu iliyofanya amjulishe tatizo hilo.

      Tofauti na Nabali, Abigaili alikuwa tayari kusikiliza

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki