-
“Moyo Uliovunjika na Kupondwa” Unapotafuta MsamahaMnara wa Mlinzi—2010 | Mei 1
-
-
Ili kumzuia Daudi asijitetee, Nathani anasimulia hadithi ambayo bila shaka ingegusa moyo wa Daudi ambaye zamani alikuwa mchungaji wa kondoo. Ni hadithi ya wanaume wawili, mmoja ni tajiri na yule mwingine ni maskini. Yule mwanamume tajiri alikuwa na “kondoo na ng’ombe wengi sana,” lakini yule mwanamume maskini “hakuwa na chochote isipokuwa mwana-kondoo jike mmoja.” Yule mwanamume tajiri alimkaribisha mgeni na alitaka kumtayarishia chakula. Badala ya kuchukua mmoja kati ya kondoo wake, alichukua yule mwana-kondoo jike mmoja wa mwanamume maskini. Inaelekea Daudi anafikiri kwamba hadithi hiyo ni ya kweli, naye anakasirika sana na kusema hivi bila kufikiri: “Mtu huyo aliyefanya hivyo anastahili kufa!” Kwa nini? Daudi anaeleza: “Kwa sababu hakuwa na huruma.”a—Mstari wa 2-6.
-
-
“Moyo Uliovunjika na Kupondwa” Unapotafuta MsamahaMnara wa Mlinzi—2010 | Mei 1
-
-
a Mtu aliyemtayarishia mgeni mwana-kondoo wa kula alionyesha sifa ya ukaribishaji-wageni. Lakini mtu aliyeiba mwana-kondoo alifanya uhalifu, na hivyo aliadhibiwa kwa kulipa kondoo wanne. (Kutoka 22:1) Kwa maoni ya Daudi, mtu huyo tajiri ambaye alichukua mwana-kondoo wa maskini hakuwa na huruma. Kwa hiyo, tajiri huyo aliiba mnyama wa yule mwanamume maskini ambaye huenda angeandalia familia yake maziwa na manyoya na ambaye hata angezaa kundi kubwa la kondoo.
-