-
Nabii wa Kale Mwenye Ujumbe wa KisasaUnabii wa Isaya I—Nuru kwa Wanadamu Wote
-
-
7. Eleza hali zilizokuwa katika Yuda siku ya Isaya.
7 Isaya na familia yake waliishi nyakati za ghasia katika historia ya Yuda. Msukosuko wa kisiasa ulikuwa umeenea, rushwa ilifisidi mahakama, na unafiki uliharibu mfumo wa kidini wa jamii. Vilele vya vilima vilijaa madhabahu za miungu isiyo ya kweli. Hata baadhi ya wafalme waliunga mkono ibada ya kipagani. Kwa mfano, Ahazi aliwaruhusu raia zake washiriki katika ibada ya sanamu na hata yeye mwenyewe aliabudu sanamu, “akampitisha mwanawe motoni” katika dhabihu ya tambiko kwa Moleki, mungu wa Wakanaani.b (2 Wafalme 16:3, 4; 2 Mambo ya Nyakati 28:3, 4) Hayo yote nayo yalitendeka miongoni mwa watu waliokuwa katika uhusiano wa agano na Yehova!—Kutoka 19:5-8.
-
-
Nabii wa Kale Mwenye Ujumbe wa KisasaUnabii wa Isaya I—Nuru kwa Wanadamu Wote
-
-
b Wengine husema kuwa ‘kupitisha motoni’ labda kwamaanisha tu sherehe ya utakaso. Ingawa hivyo, yaonekana kuwa katika muktadha huu usemi huo hurejezea dhabihu halisi. Hakuna shaka yoyote kwamba Wakanaani na Waisraeli waasi-imani walizoea kudhabihu watoto.—Kumbukumbu la Torati 12:31; Zaburi 106:37, 38.
-