-
Aliwatetea Watu wa MunguIgeni Imani Yao
-
-
19. Hamani alitaka kufanya nini, na alifanikiwaje kumshawishi mfalme?
19 Hamani alikasirika. Lakini hakutaka kumwangamiza Mordekai peke yake. Alitaka kuwaangamiza watu wote wa Mordekai! Hamani alimshawishi mfalme aamini kwamba Wayahudi ni watu wabaya. Bila kuwataja, alisema wao si watu muhimu na kwamba “wa[me]tawanyika na kujitenga kati ya vikundi vya watu.” Hata alisema hawakutii sheria za mfalme; na hivyo, walikuwa waasi hatari. Kisha, akajitolea kutoa mchango mkubwa kwa hazina ya mfalme ili kusaidia kazi ya kuwaua Wayahudi wote katika milki hiyo.d Ahasuero akampa Hamani pete yake ya kifalme ya mhuri ili atie mhuri amri yoyote aliyotaka itekelezwe.—Esta 3:5-10.
-
-
Aliwatetea Watu wa MunguIgeni Imani Yao
-
-
d Hamani alitoa mchango wa talanta 10,000 za fedha, kiasi ambacho leo ni sawa na mamilioni ya dola. Ikiwa Ahasuero alikuwa Shasta wa Kwanza, basi huenda pesa hizo zilimchochea akubali pendekezo la Hamani. Shasta alihitaji pesa nyingi ili apigane na Wagiriki katika vita vilivyosababisha uharibifu mkubwa.
-