Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Uaminifu-Maadili wa Ayubu Wathawabishwa
    Mnara wa Mlinzi—1998 | Mei 1
    • Kwanza, Yehova alimkaripia Elifazi, Bildadi, na Zofari. Akisema na Elifazi, ambaye kwa wazi ndiye aliyekuwa mwenye umri mkubwa zaidi, alisema hivi: “Hasira zangu zinawaka juu yako, na juu ya hao rafiki zako wawili; kwa kuwa ninyi hamkunena yaliyo sawa katika habari zangu, kama alivyonena mtumishi wangu Ayubu. Basi sasa, jitwalieni ng’ombe waume saba, na kondoo waume saba, mkamwendee mtumishi wangu Ayubu, mjisongezee sadaka ya kuteketezwa; na huyo mtumishi wangu Ayubu atawaombea ninyi.” (Ayubu 42:7, 8) Ebu wazia kilichodokezwa na usemi huo!

      Yehova aliwataka Elifazi, Bildadi, na Zofari watoe dhabihu kubwa, labda ili kuwakazia uzito wa dhambi yao. Kwa kweli, ama kwa kukusudia ama bila kukusudia, walikuwa wamemkufuru Mungu kwa kusema kwamba yeye ‘hana imani katika watumishi wake’ na kwamba kwa kweli halikuwa jambo la maana kwa Mungu kama Ayubu alikuwa mwaminifu au la. Elifazi hata alisema kwamba machoni pa Mungu, Ayubu hakuwa mwenye thamani zaidi ya nondo! (Ayubu 4:18, 19; 22:2, 3) Si ajabu kwamba Yehova alisema hivi: “Ninyi hamkunena yaliyo sawa katika habari zangu”!

      Lakini kuna mengi zaidi. Elifazi, Bildadi, na Zofari pia walifanya dhambi dhidi ya Ayubu binafsi, kwa kumwambia kwamba yeye mwenyewe ndiye aliyesababisha matatizo yake. Mashtaka yao yasiyo na msingi na yaliyokosa hisia-mwenzi, yalimwacha Ayubu akiwa mwenye uchungu na mwenye kushuka moyo, yakimfanya apaaze kilio hivi: “Je! mtanichukiza nafsi yangu hata lini?” (Ayubu 10:1; 19:2) Ebu wazia nyuso zenye aibu za wanaume hao watatu, kwa kuwa sasa walipaswa kumtolea Ayubu toleo kwa sababu ya dhambi zao!

      Lakini Ayubu hakupaswa kufurahia kutwezwa kwao. Kwa kweli, Yehova alimtaka asali kwa niaba ya washtaki wake. Ayubu alifanya tu vile alivyoagizwa afanye, naye alibarikiwa kwa sababu ya kufanya hivyo. Kwanza, Yehova aliponya maradhi yake yenye kuogopwa. Kisha, ndugu, dada, na washiriki wa Ayubu wa zamani wakaja kumfariji, “kila mtu akampa kipande cha fedha, na pete ya dhahabu kila mmoja.”a Isitoshe, Ayubu ‘alipata kuwa na kondoo kumi na nne elfu, na ngamia elfu sita, na jozi za ng’ombe elfu, punda wake elfu.’b Na kwa kweli mke wa Ayubu alipatanishwa naye. Halafu, Ayubu akabarikiwa kuwa na wana saba na binti watatu, naye aliishi kuviona vizazi vinne vya uzao wake.—Ayubu 42:10-17.

  • Uaminifu-Maadili wa Ayubu Wathawabishwa
    Mnara wa Mlinzi—1998 | Mei 1
    • Kabla ya kumrudishia hali nzuri ya afya, Yehova alimtaka Ayubu asali kwa niaba ya wale waliofanya dhambi dhidi yake. Ni kielelezo kizuri kama nini kwetu! Yehova hutaka kwamba tuwasamehe wale wafanyao dhambi dhidi yetu kabla ya dhambi zetu wenyewe kuweza kusamehewa. (Mathayo 6:12; Waefeso 4:32) Ikiwa hatuko tayari kuwasamehe wengine kunapokuwa na msingi mzuri wa kufanya hivyo, je, twaweza kwa haki kumtarajia Yehova atuonyeshe rehema?—Mathayo 18:21-35.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki