-
Uaminifu-Maadili wa Ayubu WathawabishwaMnara wa Mlinzi—1998 | Mei 1
-
-
Lakini Ayubu hakupaswa kufurahia kutwezwa kwao. Kwa kweli, Yehova alimtaka asali kwa niaba ya washtaki wake. Ayubu alifanya tu vile alivyoagizwa afanye, naye alibarikiwa kwa sababu ya kufanya hivyo. Kwanza, Yehova aliponya maradhi yake yenye kuogopwa. Kisha, ndugu, dada, na washiriki wa Ayubu wa zamani wakaja kumfariji, “kila mtu akampa kipande cha fedha, na pete ya dhahabu kila mmoja.”a Isitoshe, Ayubu ‘alipata kuwa na kondoo kumi na nne elfu, na ngamia elfu sita, na jozi za ng’ombe elfu, punda wake elfu.’b Na kwa kweli mke wa Ayubu alipatanishwa naye. Halafu, Ayubu akabarikiwa kuwa na wana saba na binti watatu, naye aliishi kuviona vizazi vinne vya uzao wake.—Ayubu 42:10-17.
-
-
Uaminifu-Maadili wa Ayubu WathawabishwaMnara wa Mlinzi—1998 | Mei 1
-
-
a Thamani ya “kipande cha fedha” (Kiebrania, qesi·tahʹ) haiwezi kujulikana. Lakini wakati wa Yakobo, “vipande mia vya fedha” vilinunua eneo kubwa la shamba. (Yoshua 24:32) Kwa hiyo, yaelekea “kipande cha fedha” kutoka kwa kila mgeni kilikuwa zawadi kubwa.
-