Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w97 12/15 uku. 32
  • Kurembwa kwa Kipuli cha Dhahabu

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kurembwa kwa Kipuli cha Dhahabu
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1997
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1997
w97 12/15 uku. 32

Kurembwa kwa Kipuli cha Dhahabu

TANGU nyakati za mapema zaidi, vito vya dhahabu vimethaminiwa sana kwa sababu ya ubora na uzuri wake. Alipopata kuwa waziri mkuu wa Misri, Yosefu alipokea mkufu wa dhahabu kutoka kwa Farao. (Mwanzo 41:42) Rebeka alipewa pete ya puani ya dhahabu na vikuku viwili vya dhahabu, vyenye thamani ya karibu dola 1,400 (za Marekani) katika thamani za leo. (Mwanzo 24:22) Bila shaka, zawadi hizo zenye thamani zilipokewa kwa shukrani na kuvaliwa kwa upendezi.

Biblia husema juu ya vito vya kitamathali ambavyo ni vya thamani zaidi kuliko vile vilivyovaliwa na Yosefu na Rebeka. Andiko la Mithali 25:12 lataarifu hivi: “Kipuli cha dhahabu, na pambo la dhahabu safi; ndivyo alivyo mwonyaji mwenye hekima kwa sikio lisikialo.” Mshauri atoapo shauri lenye kutegemea Neno la Mungu badala ya kutegemea kauli yake mwenyewe, kwa kweli anatoa zawadi yenye thamani. Kwa nini? Kwa sababu shauri hilo hasa latoka kwa Yehova mwenyewe. Biblia hutuambia hivi: “Mwanangu, usidharau kuadhibiwa na BWANA, wala usione ni taabu kurudiwa naye. Kwa kuwa BWANA ampendaye humrudi, kama vile baba mwanawe ampendezaye.” (Mithali 3:11, 12) Msikilizaji apokeapo na kutumia hilo shauri kwa unyenyekevu, yu kana kwamba anajiremba kwa kipuli cha dhahabu. Ni kama vile mithali ya Biblia iliyopuliziwa isemavyo: “Heri mtu yule aonaye hekima, na mtu yule apataye ufahamu. Maana biashara yake ni bora kuliko biashara ya fedha, na faida yake ni nyingi kuliko dhahabu safi.”—Mithali 3:13, 14.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki