Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Maswali Kutoka kwa Wasomaji
    Mnara wa Mlinzi—1991 | Agosti 1
    • Kitabu cha Mithali kina mistari mingi ambayo peke yayo ni taarifa za shauri zenye maana, lakini Mithali 27:23 ni sehemu ya kikundi cha mistari: “Fanya bidii kuijua hali ya makundi yako; na kuwaangalia sana ng’ombe zako. Kwa maana mali haziwi za milele; na taji je! yadumu tangu kizazi hata kizazi? Manyasi huchukuliwa, na majani mabichi huonekana, na maboga ya milimani hukusanyika. Wana-kondoo hufaa kwa mavazi yako; na mbuzi ni thamani ya shamba: Tena yatakuwapo maziwa ya mbuzi, ya kukutosha kwa chakula chako, na chakula cha watu wa nyumbani mwako, na posho la vijakazi vyako.”—Mithali 27:23-27.

  • Maswali Kutoka kwa Wasomaji
    Mnara wa Mlinzi—1991 | Agosti 1
    • “Mali,” au utajiri upatwao katika shughuli za biashara za haraka-haraka, zikitokeza umashuhuri (“taji”), zaweza kutokomea kwa urahisi, kama vile wengi waweza kushuhudia. Kwa hiyo, kuna mengi ya kusema kwa maisha rahisi, kama yale yaliyofuatwa na wachungaji wa zamani katika kutunza wanyama. Njia hiyo ya maisha haikuwa rahisi katika maana ya kuwa bila daraka lolote. Mchungaji alihitaji kuwa na ufikirio kwa kundi lake, akihakikisha kwamba kondoo walilindwa. (Zaburi 23:4) Ikiwa, alipokuwa akiwachunguza, angepata kondoo aliyekuwa mgonjwa au aliyejeruhiwa, angeweza kumpaka mafuta yenye kutuliza. (Zaburi 23:5; Ezekieli 34:4; Zekaria 11:16) Katika hali zilizo nyingi mchungaji mwenye bidii-nyendelevu aliyehangaikia makundi yake kwa moyo angeona jitihada zake zikiwa na matokeo—ongezeko la polepole la kundi lake.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki