-
Maswali Kutoka kwa WasomajiMnara wa Mlinzi—1991 | Agosti 1
-
-
Kitabu cha Mithali kina mistari mingi ambayo peke yayo ni taarifa za shauri zenye maana, lakini Mithali 27:23 ni sehemu ya kikundi cha mistari: “Fanya bidii kuijua hali ya makundi yako; na kuwaangalia sana ng’ombe zako. Kwa maana mali haziwi za milele; na taji je! yadumu tangu kizazi hata kizazi? Manyasi huchukuliwa, na majani mabichi huonekana, na maboga ya milimani hukusanyika. Wana-kondoo hufaa kwa mavazi yako; na mbuzi ni thamani ya shamba: Tena yatakuwapo maziwa ya mbuzi, ya kukutosha kwa chakula chako, na chakula cha watu wa nyumbani mwako, na posho la vijakazi vyako.”—Mithali 27:23-27.
-
-
Maswali Kutoka kwa WasomajiMnara wa Mlinzi—1991 | Agosti 1
-
-
Mchungaji mwenye bidii na aliye mwangalifu alikuwa na chanzo cha msaada chenye kutegemeka—Yehova. Jinsi gani? Mungu huandaa majira na mirudio ambayo hutokeza kwa kawaida manyasi ya kutosha ambayo yangeweza kulisha kundi. (Zaburi 145:16) Wakati, kwa mabadiliko ya majira, manyasi mabichi hutoweka katika mikoa ya chini, yanaweza kuwa tele kwenye sehemu zilizoinuka zaidi, ambapo mchungaji mwenye uangalifu angeweza kuhamisha wanyama wake.
-