Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Je, Kazi Yako Itastahimili Moto?
    Mnara wa Mlinzi—1998 | Novemba 1
    • 4. (a) Paulo alikuwa na fungu gani katika kazi ya Kikristo ya kujenga? (b) Kwa nini yaweza kusemwa kwamba Yesu na pia wasikilizaji wake walijua umuhimu wa misingi ifaayo?

      4 Ikiwa jengo litakuwa imara na lenye kudumu, lahitaji msingi ufaao. Hivyo, Paulo aliandika: “Kulingana na fadhili isiyostahiliwa ya Mungu niliyopewa, kama mwelekezi wa kazi za ufundi mwenye hekima niliweka msingi.” (1 Wakorintho 3:10) Akitumia kielezi sawa na hicho, Yesu Kristo alisimulia juu ya nyumba iliyookoka dhoruba kwa sababu mjenzi wake alikuwa amechagua msingi imara. (Luka 6:47-49) Yesu alijua yote kuhusu umuhimu wa misingi. Alikuwepo Yehova alipoweka msingi wa dunia.a (Mithali 8:29-31) Waliomsikiliza Yesu pia walithamini misingi ifaayo. Nyumba zenye misingi ifaayo pekee ndizo zingeweza kuokoka mafuriko ya ghafula na matetemeko ya dunia ambayo nyakati nyingine yalitokea huko Palestina. Ingawa hivyo, Paulo alikuwa akifikiria msingi upi?

  • Je, Kazi Yako Itastahimili Moto?
    Mnara wa Mlinzi—1998 | Novemba 1
    • a Huenda ‘msingi wa dunia’ ukawa warejezea nguvu za asili zinazoshikilia dunia imara—na sayari zote—mahali pake. Kwa kuongezea, dunia yenyewe imefanyizwa katika njia ya kwamba ‘haitatikisika,’ au kupatwa na uharibifu.—Zaburi 104:5.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki