Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • “Kwa Jumla Ndiyo Impasayo Mtu”
    Mnara wa Mlinzi—1997 | Februari 15
    • 13. (a) Mhubiri 9:4, 5 hutusaidiaje tuwe na maoni yafaayo juu ya kujitahidi kupata umashuhuri au mamlaka? (b) Twapaswa kukabili mambo gani ya hakika ikiwa uhai ndio uu huu tu? (Ona kielezi-chini.)

      13 Umashuhuri au mamlaka hiyo ina tokeo gani hatimaye? Kizazi kimoja kipitapo na kingine kuja, watu mashuhuri au wenye mamlaka wanakufa na kusahauliwa. Ndivyo ilivyo kwa habari ya wajenzi, wanamuziki, na mafundi wengine, wanamapinduzi wa kijamii, na kadhalika, jinsi ilivyo kweli kwa habari ya wanasiasa walio wengi na viongozi wa kijeshi. Kati ya shughuli hizo, unajua watu wangapi hususa walioishi kati ya mwaka wa 1700 na wa 1800? Solomoni alikadiria mambo ifaavyo, akisema hivi: “Ni afadhali mbwa aliye hai kuliko simba aliyekufa; kwa sababu walio hai wanajua ya kwamba watakufa; lakini wafu hawajui neno lo lote, . . . kumbukumbu lao limesahauliwa.” (Mhubiri 9:4, 5) Na ikiwa uhai ndio uu huu tu, basi kujitahidi ili kupata umashuhuri au mamlaka ni ubatili kikweli.a

  • “Kwa Jumla Ndiyo Impasayo Mtu”
    Mnara wa Mlinzi—1997 | Februari 15
    • a Wakati mmoja Mnara wa Mlinzi (la Kiingereza) lilitoa maelezo haya yenye ufahamu wenye kina: “Hatupaswi kutumia vibaya uhai huu katika mambo ya ubatili . . . Ikiwa uhai ndio uu huu tu, hakuna jambo la maana. Uhai huu ni kama mpira utupwao hewani ambao waanguka upesi mavumbini tena. Ni kivuli kipitacho upesi, ua linalofifia, unyasi wa kukatwa na kunyauka upesi. . . . Kwenye kipimio cha umilele urefu wa uhai wetu ni chembe ya kupuuzwa. Huo hata si tone kubwa katika mkondo wa wakati. Kwa uhakika [Solomoni] asema kweli anapopitia mahangaiko na utendaji mwingi wa kibinadamu maishani na kuziita ubatili. Tunakufa upesi sana hivi kwamba yafaa tusingalizaliwa, mmojawapo mabilioni anayezaliwa na kufa, kukiwa na wachache sana wakijua kwamba tulipata kuwako. Maoni hayo si ya kudharau au ya kushusha moyo au ya majonzi au ya kuhuzunisha. Ni ya kweli, mambo ya hakika, maoni halisi, ikiwa uhai ndio uu huu tu.”—Agosti 1, 1957, ukurasa 472.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki