Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Ole kwa Shamba la Mizabibu Lisilo na Uaminifu!
    Unabii wa Isaya I—Nuru kwa Wanadamu Wote
    • 4 Kazi ngumu yahitajika ili shamba la mizabibu lizae. Isaya aeleza kuwa mmilikaji ‘afanya handaki [“alililima vizuri,” BHN] shamba na kutoa mawe yake’—kazi ngumu, yenye kuchosha sana! Yaelekea atumia mawe yaliyo makubwa ‘kujenga mnara.’ Nyakati za kale, minara hiyo ilikuwa vituo vya walinzi walioilinda mimea dhidi ya wezi na wanyama.a Pia, ajenga ukuta wa mawe ili kuyazunguka matuta ya shamba hilo la mizabibu. (Isaya 5:5) Mara nyingi hilo lilifanywa ili kuzuia mmomonyoko wa udongo wa juu ulio muhimu.

  • Ole kwa Shamba la Mizabibu Lisilo na Uaminifu!
    Unabii wa Isaya I—Nuru kwa Wanadamu Wote
    • 6, 7. (a) Ni nani aliye mmilikaji wa shamba la mizabibu, na shamba la mizabibu ni nini? (b) Mmilikaji aomba hukumu gani ifanywe?

      6 Mmilikaji ni nani, nalo shamba la mizabibu ni nini? Mmilikaji wa shamba la mizabibu ajibu maswali hayo anaposema: “Sasa, enyi wenyeji wa Yerusalemu, nanyi watu wa Yuda, amueni, nawasihi, kati ya mimi na shamba langu la mizabibu. Je! ni kazi gani iliyoweza kutendeka ndani ya shamba langu la mizabibu nisiyoitenda? Basi, nilipotumaini ya kuwa litazaa zabibu, mbona lilizaa zabibu-mwitu? Haya basi, sasa nitawaambieni nitakalolitenda shamba langu la mizabibu; nitaondoa kitalu [“ua wa miti,” “NW”] chake, nalo litaliwa; nitabomoa ukuta wake, nalo litakanyagwa.”—Isaya 5:3-5.

  • Ole kwa Shamba la Mizabibu Lisilo na Uaminifu!
    Unabii wa Isaya I—Nuru kwa Wanadamu Wote
    • 9. Yehova amelitunzaje taifa lake kama shamba la mizabibu lenye kuthaminiwa?

      9 Yehova ‘alilipanda’ taifa lake katika nchi ya Kanaani na kuwapa sheria na kanuni zake, zilizokuwa kama ukuta wa kuwalinda ili mataifa mengine yasiwafisidi. (Kutoka 19:5, 6; Zaburi 147:19, 20; Waefeso 2:14) Pamoja na hayo, Yehova aliwapa waamuzi, makuhani, na manabii wa kuwafundisha. (2 Wafalme 17:13; Malaki 2:7; Matendo 13:20) Israeli ilipotishwa kwa uvamizi wa kijeshi, Yehova aliinua wakombozi. (Waebrania 11:32, 33) Kwa kufaa, Yehova auliza: “Je! ni kazi gani iliyoweza kutendeka ndani ya shamba langu la mizabibu nisiyoitenda?”

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki