-
“Na Tunyoshe Mambo”Unabii wa Isaya I—Nuru kwa Wanadamu Wote
-
-
1, 2. Yehova awalinganisha na nani watawala na watu wa Yerusalemu na Yuda, na kwa nini ulinganisho huo wastahili?
HUENDA wakazi wa Yerusalemu wakataka kujitetea baada ya kusikia shutumu la hadharani kama ilivyorekodiwa katika Isaya 1:1-9. Yamkini wangetaka kutaja kwa majivuno zile dhabihu zote wanazomtolea Yehova. Hata hivyo, mstari wa 10 hadi wa 15 hutoa jibu la Yehova linalolaumu vikali mitazamo hiyo. Laanza hivi: “Lisikieni neno la BWANA, enyi waamuzi wa Sodoma; tegeni masikio msikie sheria ya Mungu wetu, enyi watu wa Gomora.”—Isaya 1:10.
2 Sodoma na Gomora yaliharibiwa, si kwa sababu ya mazoea yao mapotovu ya kingono tu, bali pia kwa sababu ya mitazamo yao ya ugumu wa moyo na yenye kiburi. (Mwanzo 18:20, 21; 19:4, 5, 23-25; Ezekieli 16:49, 50) Watu wanaomsikiliza Isaya lazima wanashtuka kusikia wakilinganishwa na watu wa majiji hayo yaliyolaaniwa.a Lakini Yehova awaona watu wake jinsi walivyo, naye Isaya hapunguzi uzito wa ujumbe wa Mungu ili ‘kutekenya masikio yao.’—2 Timotheo 4:3.
-
-
“Na Tunyoshe Mambo”Unabii wa Isaya I—Nuru kwa Wanadamu Wote
-
-
a Kwa mujibu wa mapokeo ya kale ya Wayahudi, Mfalme Manase mwovu alifanya Isaya auawe, akatwe vipande-vipande kwa msumeno. (Linganisha Waebrania 11:37.) Chanzo kimoja chasema kuwa nabii fulani asiye wa kweli alileta mashtaka yafuatayo juu ya Isaya, ili apewe adhabu hiyo ya kifo: “Ameliita Yerusalemu Sodoma, naye amewatangaza wakuu wa Yuda na Yerusalemu (kuwa) watu wa Gomora.”
-