Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Unafiki Wafichuliwa!
    Unabii wa Isaya II—Nuru kwa Wanadamu Wote
    • 8, 9. Ni vitendo gani vinavyofaa vinavyopaswa kuandamana na toba ya moyo mweupe?

      8 Licha ya Yehova kutaka watu wake wafunge kwa sababu ya dhambi zao, anataka watubu pia. Kisha watapata kibali chake. (Ezekieli 18:23, 32) Anaeleza kwamba kufunga kunaweza kuwa na maana ikiwa pia dhambi za wakati uliopita zitarekebishwa. Yafikirie maswali ya kupekua moyo ambayo Yehova anauliza: “Je! saumu niliyoichagua, siyo ya namna hii? kufungua vifungo vya uovu, kuzilegeza kamba za nira, kuwaacha huru walioonewa, na kwamba mvunje kila nira?”—Isaya 58:6.

      9 Vifungo na nira ni ishara zinazofaa sana za utumwa mkatili. Kwa hiyo, badala ya kufunga na huku wanawakandamiza waamini wenzao, watu hao wanapaswa kutii amri hii: “Umpende jirani yako kama nafsi yako.” (Mambo ya Walawi 19:18) Wanapaswa kuwafungua watu wote ambao wao wamewakandamiza na kuwatumikisha bila haki.a Vitendo vya kidini vya kujionyesha, kama vile kufunga kula, haviwezi kuchukua mahali pa ujitoaji halisi wa kimungu. Wala haviwezi kuchukua mahali pa vitendo vinavyoonyesha upendo wa kidugu. Nabii Mika, mtu aliyeishi wakati mmoja na Isaya, anaandika hivi: “BWANA anataka nini kwako, ila kutenda haki, na kupenda rehema, na kwenda kwa unyenyekevu na Mungu wako!”—Mika 6:8.

  • Unafiki Wafichuliwa!
    Unabii wa Isaya II—Nuru kwa Wanadamu Wote
    • a Yehova aliwafanyia watu wake uandalizi wa kujiuza utumwani iwapo walitumbukia katika deni—wakawa hasa wafanya-kazi wa kuajiriwa—ili kulipia madeni yao. (Mambo ya Walawi 25:39-43) Hata hivyo, Sheria ilitaka kwamba watumwa watendewe fadhili. Wale waliotendwa ukatili walipaswa kuachiliwa huru.—Kutoka 21:2, 3, 26, 27; Kumbukumbu la Torati 15:12-15.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki