Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Ibada ya Kweli Yapanuka Ulimwenguni Pote
    Unabii wa Isaya II—Nuru kwa Wanadamu Wote
    • 11, 12. (a) Yule “mwanamke” anaona nini anapokaza macho magharibi? (b) Kwa nini watu wengi sana wanafanya haraka kwenda Yerusalemu?

      11 Sasa Yehova anamwagiza yule “mwanamke” atazame kwenye upeo wa magharibi. Halafu Yehova anauliza: “Ni nani hawa warukao kama wingu, na kama njiwa waendao madirishani kwao?” Yehova mwenyewe anajibu hivi: “Hakika yake visiwa vitaningojea, na merikebu za Tarshishi kwanza, ili kuleta wana wako kutoka mbali, na fedha yao na dhahabu yao pamoja nao, kwa ajili ya jina la BWANA, Mungu wako, kwa ajili yake Mtakatifu wa Israeli, kwa kuwa amekutukuza wewe.”—Isaya 60:8, 9.

      12 Wazia kwamba umesimama pamoja na “mwanamke” huyo, ukikaza macho magharibi ng’ambo ya Bahari Kuu. Unaona nini? Wingu la mbali la madoa meupe yakielea juu ya maji. Wanaonekana kama ndege. Lakini wanapokaribia zaidi, unaona kwamba kumbe ni merikebu zenye matanga yaliyotwekwa. ‘Zimekuja kutoka mbali.’a (Isaya 49:12) Mashua zinazoenda kasi kuelekea Sayuni ni nyingi sana hivi kwamba zinaonekana kama kundi la njiwa wanaoelekea nyumbani. Haraka yote hiyo ya nini? Kikosi hicho kina hamu nyingi ya kuwafikisha pwani waabudu wa Yehova waliomo, ambao wametoka bandari za mbali. Kwa kweli, wote wale wanaowasili sasa hivi—Waisraeli na wageni pia, kutoka mashariki au magharibi na kutoka nchi za karibu au za mbali—wanafanya haraka kwenda Yerusalemu wakafanye vitu vyote walivyo navyo viwe wakfu kwa jina la Yehova, Mungu wao.—Isaya 55:5.

  • Ibada ya Kweli Yapanuka Ulimwenguni Pote
    Unabii wa Isaya II—Nuru kwa Wanadamu Wote
    • a Yaelekea kwamba Tarshishi ilikuwa mahali panapojulikana sasa kuwa Hispania. Hata hivyo, kulingana na vitabu fulani vya marejeo, usemi “merikebu za Tarshishi” unamaanisha aina ya merikebu zinazotumika, yaani “vyombo vya usafiri wa baharini vyenye milingoti mirefu” ambavyo “vilifaa kuenda-enda Tarshishi.” Maana yake, merikebu hizo zilionwa kuwa zinafaa kusafiri-safiri mwendo mrefu hadi bandari za mbali.—1 Wafalme 22:48.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki