Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Yehova Ajifanyia Jina Maridadi
    Unabii wa Isaya II—Nuru kwa Wanadamu Wote
    • 12, 13. (a) Ni kwa njia gani Yehova hana msaidiaji? (b) Mkono wa Yehova unaandaje wokovu, na ghadhabu yake inamtegemezaje?

      12 Yehova anaendelea kusema hivi: “Nikatazama, wala hakuna wa kusaidia; nikashangaa kwa kuwa hakuna mwenye kutegemeza; basi, mkono wangu mwenyewe uliniletea wokovu, ghadhabu yangu ndiyo iliyonitegemeza. Nikazikanyaga kabila za watu kwa hasira yangu, nikawalevya kwa ghadhabu yangu, nami nikaimwaga damu yao [“inayofoka-foka,” “NW”] chini.”—Isaya 63:5, 6.

      13 Hakuna msaidiaji wa kibinadamu anayeweza kudai sifa ya kuleta ile siku kuu ya kisasi cha Yehova. Wala Yehova hahitaji utegemezo wowote wa kibinadamu ili kutimiza mapenzi yake.c Mkono wake wenye nguvu unaiweza kazi iliyopo. (Zaburi 44:3; 98:1; Yeremia 27:5) Isitoshe, ghadhabu yake inamtegemeza. Kwa njia gani? Kwa maana ya kwamba ghadhabu ya Mungu si hisia-moyo isiyodhibitiwa, bali ni hasira ya haki. Kwa kuwa sikuzote Yehova huchukua hatua zinazotegemea kanuni za uadilifu, ghadhabu yake inamwunga mkono na kumchochea ‘kumwaga chini’ ile ‘damu inayofoka-foka’ ya adui zake, hata kuwashushia heshima na kuwashinda.—Zaburi 75:8; Isaya 25:10; 26:5.

  • Yehova Ajifanyia Jina Maridadi
    Unabii wa Isaya II—Nuru kwa Wanadamu Wote
    • c Yehova anasema anastaajabu kwamba hakuna mtu aliyejitolea kumwunga mkono. Kweli ingeweza kustaajabisha kwamba karibu miaka 2,000 baada ya kifo cha Yesu, wenye mamlaka miongoni mwa wanadamu wangali wanapinga mapenzi ya Mungu.—Zaburi 2:2-12; Isaya 59:16.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki