Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Ole Wao Waasi!
    Unabii wa Isaya I—Nuru kwa Wanadamu Wote
    • 1. Yeroboamu alifanya kosa gani kubwa?

      WATU wa Yehova wa agano walipogawanyika na kuwa falme mbili, ufalme wa kaskazini wa makabila kumi ukawa chini ya utawala wa Yeroboamu. Mfalme huyo mpya alikuwa mtawala mwenye uweza na nguvu. Lakini hakuwa na imani kamili katika Yehova. Kwa sababu hiyo alifanya kosa kubwa lililoathiri vibaya historia yote ya ufalme wa kaskazini. Sheria ya Kimusa iliwaamuru Waisraeli wafunge safari mara tatu kwa mwaka ya kwenda hekaluni huko Yerusalemu, jiji ambalo sasa lilikuwa katika ufalme wa kusini wa Yuda. (Kumbukumbu la Torati 16:16) Akihofia kuwa safari hizo za kawaida zingewafanya raia zake wafikirie kuhusu kuungana tena na ndugu zao wa kusini, Yeroboamu “a[li]fanyiza ng’ombe wawili wa dhahabu, akawaambia watu, Ni vigumu kwenu kupanda kwenda Yerusalemu; tazama, hii ndiyo miungu yenu, enyi Israeli, iliyowapandisha kutoka nchi ya Misri. Akamweka mmoja katika Betheli, na wa pili akamweka katika Dani.”—1 Wafalme 12:28, 29.

      2, 3. Kosa la Yeroboamu liliathirije Israeli?

      2 Kwa muda fulani, ilionekana kwamba mpango wa Yeroboamu umefanikiwa. Hatua kwa hatua watu wakaacha kwenda Yerusalemu nao wakaanza kuabudu mbele ya ng’ombe hao wawili. (1 Wafalme 12:30) Hata hivyo, zoea hilo la kidini la uasi lilifisidi ufalme wa kaskazini wa makabila kumi. Miaka iliyofuata, hata Yehu, aliyekuwa amefanya bidii yenye kustahili pongezi ya kuondolea mbali ibada ya Baali katika Israeli, aliendelea kuinamia ndama hao wa dhahabu. (2 Wafalme 10:28, 29) Uamuzi mbaya sana wa Yeroboamu ulisababisha mambo gani mengine? Misukosuko ya kisiasa na watu kuteseka.

      3 Kwa sababu ya uasi wa Yeroboamu, Yehova alisema kuwa uzao wake haungetawala katika nchi hiyo, na mwishowe msiba mbaya sana ungeukumba ufalme wa kaskazini. (1 Wafalme 14:14, 15) Neno la Yehova likatimia kweli. Wafalme saba kati ya wafalme wa Israeli walitawala kwa miaka miwili au kwa muda usiozidi huo—baadhi yao kwa siku chache tu. Mfalme mmoja alijiua, na sita wakauawa na watu wenye tamaa ya makuu walionyakua kiti cha ufalme. Hasa baada ya utawala wa Yeroboamu wa Pili, uliokwisha karibu mwaka wa 804 K.W.K. huku Uzia akitawala katika Yuda, Israeli ilikumbwa na ghasia, jeuri, na mauaji. Kwa sababu ya hali hizo, Yehova apeleka onyo, au “neno,” la moja kwa moja kupitia Isaya kwa ufalme wa kaskazini. “Bwana alimpelekea Yakobo neno, likamfikilia Israeli.”—Isaya 9:8.a

  • Ole Wao Waasi!
    Unabii wa Isaya I—Nuru kwa Wanadamu Wote
    • a Isaya 9:8–10:4 ina beti nne (mafungu ya shairi), kila mmoja ukimalizika kwa kibwagizo chenye kutisha: “Pamoja na hayo yote hasira yake haikugeukia mbali, lakini mkono wake umenyoshwa hata sasa.” (Isaya 9:12, 17, 21; 10:4) Mtindo huo wa kifasihi huunganisha Isaya 9:8–10:4 kuwa “neno” moja kuu. (Isaya 9:8) Pia ona kwamba “mkono [wa Yehova] umenyoshwa hata sasa,” si kwa ajili ya kuleta upatanisho, bali kuhukumu.—Isaya 9:13.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki