Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • “Babeli Umeanguka”!
    Unabii wa Isaya I—Nuru kwa Wanadamu Wote
    • 8. Kama ilivyotabiriwa, Wababiloni watendaje, hata ingawa adui zao wako nje ya kuta?

      8 Giza liingiapo usiku huo wenye maafa, Wababiloni hawana hofu hata kidogo. Isaya atabiri hivi karne mbili mapema: “Wanaandika meza, wanaweka ulinzi, wanakula, wanakunywa.” (Isaya 21:5a) Naam, Mfalme Belshaza mwenye kiburi aandaa karamu. Viti vimepangwa kwa ajili ya wakuu wake elfu, na pia wake na masuria wengi. (Danieli 5:1, 2) Wenye kusherehekea wafahamu kuwa kuna jeshi nje ya kuta, lakini waamini kwamba jiji lao haliwezi kupenywa. Kuta zake kubwa mno na mahandaki yake ya maji yenye kina kirefu yafanya lionekane kuwa lisiloweza kamwe kutekwa; miungu yake mingi yafanya kutekwa kusiwazike hata kidogo. Basi, acha ‘wale na wanywe’! Belshaza alewa, na labda wengine pia. Ile haja ya kuwaamsha maofisa wa ngazi za juu yadokeza kuwa wamepumbazika, kama vile maneno yafuatayo ya Isaya yaonyeshavyo kwa njia ya unabii.

      9. Kwa nini kuna uhitaji wa ‘kutia ngao mafuta’?

      9 “Simameni, enyi wakuu, itieni ngao mafuta.” (Isaya 21:5b) Karamu yaisha ghafula. Yawapasa wakuu wajiamshe! Danieli, nabii mzee, ameitwa, naye aona jinsi Yehova anavyomtia hofu Mfalme Belshaza wa Babiloni, hofu kama ile ambayo Isaya alieleza. Wakuu wa mfalme wavurugika huku majeshi ya mwungano wa Wamedi, Waajemi, na Waelami yashindapo kinga za jiji. Babiloni laanguka mara moja! Lakini, ‘kutia ngao mafuta’ kwamaanisha nini? Nyakati nyingine Biblia humrejezea mfalme wa taifa kuwa ngao yake kwa sababu yeye ndiye anayekinga na kulinda nchi.b (Zaburi 89:18) Basi labda mstari huo katika Isaya watabiri uhitaji wa mfalme mpya. Kwa nini? Kwa sababu Belshaza auawa “usiku uo huo.” Kwa hiyo, kuna uhitaji wa ‘kutia ngao mafuta,’ au kumteua mfalme mpya.—Danieli 5:1-9, 30.

  • “Babeli Umeanguka”!
    Unabii wa Isaya I—Nuru kwa Wanadamu Wote
    • b Waelezaji wengi wa Biblia hufikiri kuwa maneno “itieni ngao mafuta” yarejezea zoea la zamani la kijeshi la kutia mafuta kwenye ngao zao za ngozi kabla ya vita ndipo silaha nyingi zinazorushwa ziteleze. Ingawa fasiri hiyo huenda ikawa kweli, yapasa ikumbukwe kuwa usiku ambao jiji hilo lilianguka, Wababiloni hawakuwa na wakati wa kupigana, sembuse wa kujitayarishia vita kwa kutia ngao zao mafuta!

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki