Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Jifunze Kutokana na Mfano wa Danieli
    Mnara wa Mlinzi (Funzo)—2023 | Agosti
    • 6. Huenda ni nini kilichomsaidia Danieli awe jasiri?

      6 Huenda ni nini kilichomsaidia Danieli awe jasiri katika maisha yake yote? Alipokuwa mtoto, Danieli aliiga mfano mzuri wa baba na mama yake. Bila shaka, walikuwa wametii maagizo ambayo Yehova aliwapatia wazazi Waisraeli, na walimfundisha mtoto wao Sheria ya Mungu. (Kum. 6:6-9) Danieli hakujua mambo ya msingi tu kuhusu Sheria, kama vile zile amri kumi, bali pia alijua habari nyingi kuhusu chakula ambacho Mwisraeli angeweza kula au kutokula.b (Law. 11:4-8; Dan. 1:8, 11-13) Pia, Danieli alijifunza kuhusu historia ya watu wa Mungu na alijua kilichowapata walipokosa kuishi kulingana na viwango vya Yehova. (Dan. 9:10, 11) Mambo ambayo Danieli alijionea katika maisha yake yote, yalimpa uhakika kwamba Yehova na malaika Wake wenye nguvu walikuwa wakimsaidia.​—Dan. 2:19-24; 10:12, 18, 19.

  • Jifunze Kutokana na Mfano wa Danieli
    Mnara wa Mlinzi (Funzo)—2023 | Agosti
    • b Inawezekana kwamba Danieli alikuwa na sababu tatu zilizomfanya aone chakula cha Wababiloni kuwa kisicho safi: (1) Huenda walikula nyama ya wanyama waliokatazwa kwenye Sheria. (Kum. 14:7, 8) (2) Huenda nyama hiyo haikutolewa damu vizuri. (Law. 17:10-12) (3) Huenda kula chakula hicho kungeonwa kuwa kushiriki ibada ya miungu ya uwongo.​—Linganisha Mambo ya Walawi 7:15 na 1 Wakorintho 10:18, 21, 22.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki